Tetesi zinasema, Harry Kane, 28, atasubiri hadi mwisho wa msimu kabla ya kuamua mustakabali wake wa Tottenham, huku nahodha huyo wa Uingereza kwa sasa hataki kujadili kuongezwa kwa mkataba wake.
Arsenal wamekasirishwa kufuatia kushindwa kumpata mshambuliaji wa Serbia Dusan Vlahovic, 22, huku Mikel Arteta sasa akikabiliwa na kinyang’anyiro cha kusuluhisha kitendawili cha mshambuliaji.
Real Madrid wamewasilisha ofa ya mwisho kwa mshambuliaji wa Borussia Dortmund Erling Braut Haaland, 21, ambayo inaweza kuwa pigo kwa matumaini ya Manchester United, Chelsea na Manchester City ya kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Norway.
Thomas Tuchel anasema Cesar Azpilicueta bado ni muhimu sana kwa mipango yake ya Chelsea licha ya kandarasi ya beki huyo wa Uhispania mwenye umri wa miaka 32 kumalizika.
Tetesi zinasema, Chelsea ni miongoni mwa klabu zinazomwinda kiungo wa kati wa Barcelona na Uhispania Gavi, 17.
Tetesi zinasema, Mchezaji Mwingereza Eberechi Eze, 23, ana furaha katika Crystal Palace huku kukiwa na nia kutoka Newcastle.
Tetesi zinasema, Beki wa Sevilla na Ufaransa Jules Kounde, 23, anapendelea kuhamia Chelsea ikiwa ataondoka katika klabu hiyo ya La Liga.
Kiungo wa kati wa Uholanzi Donny van de Beek, 24, atajaribu kuipa kisogo Manchester United kwa uzuri na kupata uhamisho wa kudumu wa kwenda Everton msimu huu wa joto ikiwa atawasaidia kuendelea kucheza Ligi ya Premia huku akiwa huko kwa mkopo.
Marcelo Bielsa amekataa kuzungumzia mustakabali wake huku kukiwa na uvumi iwapo atasalia kuwa kocha mkuu wa Leeds kwa msimu mwingine.
Haijawahi kuwa rahisi hivi kwenye safari yako ya kuvuna mkwanja, kasino maridhawa ya meridianbettz inakuletea mchezo wa Emoticoins unaokupa nafasi ya kufanya safari yako kuwa rahisi zaidi. Wakati ni wako nafasi ni yako na Emoticoins.