Tetesi zinasema, Manchester United imepeleka ofa ya kumsajili kiungo wa Denmark Christian Eriksen, 30, wakati huu mkataba wake na Brentford ukimalizika mwishoni mwa mwezi Juni.

Bayern Munich inajiandaa kutoa ofa ya £34.6m kwaajili mshambuliaji wa Senegal Sadio Mane, 30 baada ya Liverpool kukataa ofa mbili za awali za klabu hiyo ya Ujerumani.

Tetesi zinasema, Juventus inakaribia kumalizana na kiungo mfaransa aliyeondoka Manchester United Paul Pogba, 29.


 

Tetesi za Soka Barani Ulaya.

Manchester City inaweza kupata zaidi ya £200m kwa kuuza wachezaji msimu huu wakati klabu hiyo ikataka kumsajili kiungo wa Leeds United na England Kalvin Phillips, 26.

Tetesi zinasema, Mshambuliaji wa Everton Richarlison, 25, amekataa ofa ya kujiunga na Arsenal msimu huu huku Chelsea na Tottenham Hotspur zikitajwa kipaumbele kwa mbrazil huyo.

Inter Milan inapambama kumsajili Romelu Lukaku, 29, kutoka Chelsea, mshambuliaji huyo wa belgiji anajiandaa kukubali kupunguza mshahara ili kurejea Seeia A.

 

Lukaku Adhamiria Kurejea Inter Milan.

Leeds United imefikia makubaliano ya mdomo na kiungo wa mhispania Marc Roca, 25, kutoka Bayern Munich kwa mkataba wa miaka 4 wenye thamani ya 12m.

Chelsea wanafikiria kumnunua mlinda mlango wa kimataifa wa Lazio na Albania Thomas Strakosha, 27, ikiwa kipa wa Hispania Kepa, 27, ataondoka katika klabu hiyo msimu huu wa joto.

Winga wa Leeds Raphinha, 25, anasakwa na vilabu vya Arsenal na Tottenham Hotspur msimu huu wa joto, huku kukiwa na wasiwasi kwamba Barcelona hawataweza kumsajii Mbrazil huyo.


ALIYA’S WISHES

Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa.Kasino ya Mtandaoni

CHEZA SASA


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa