Tetesi za Soka Barani Ulaya.


Tetesi zinasema Mlinzi wa kushoto wa Real Madrid na Uhispania Sergio Reguilon ,23, yupo katika kiwanja cha mazoezi cha Tottenham kwa vipimo vya afya kabla ya kujiunga na klabu hiyo ya Ligi kuu.

Kocha wa Everton Carlo Ancelotti anataka kumsajili mchezaji wa nafasi ya ulinzi wa Chelsea Fikayo Tomori, 22, lakini pia yuko tayari kuwaachia wachezaji kadhaa akiwemo viungo wa kati Gylfi Sigurdsson, 31, na Fabian Delph , 30 .

Manchester City wanajiandaa kuwa uhamisho wa mchezaji wa nafasi ya ulinzi anayekipiga Atletico Madrid, Jose Gimenez, ikiwa Napoli itakataa kushusha dau kwa ajili ya mlinzi wa kati Kalidou Koulibaly,29.

 

Tetesi za Soka Barani Ulaya.

Kiungo mkabaji wa Atletico Madrid Thomas Partey,27, ni miongoni mwa wachezaji wanaolengwa na Arsenal lakini klabu hiyo ya Uhispania watamuuza tu iwapo dau la pauni milioni 45 litafikiwa.

Manchester United inaangalia uwezekano wa kumsajili winga wa kulia wa Ivory Coast Amad Traore,18, kutoka Atalanta.

Tetesi zinasema Leicester City wako karibuni kumsajili winga wa Roma Cengiz Under.

Tetesi zinasema Kocha wa Barcelona Ronald Koeman amesema kuwa timu hiyo haitamrejesha mlinzi wa Manchester City, Mhispania Eric Garcia,19.

Tetesi zinasema Arsenal inamfuatilia mlinda mlango wa Dijon Runar Alex Runarsson, 25, huku washika bunduki hao wakiwa na matumaini makubaliano ya dau la pauni milioni 1.5 litafikiwa.

 

Tetesi za Soka Barani Ulaya.

Rais wa Lyon Jean-Michel Aulas amekana ripoti kuwa mchezaji wa nafasi ya kiungo wa kati,Memphis Depay, aliyekuwa akichezea Manchester United, yuko njiani kujiunga na Barcelona.

Tetesi zinasema Sheffield United imemfuatilia mshambuliji wa Arsenal Folarin Balogun, 19, Kocha Chris Wilder amethibitisha.

RB Leipzig imetishia kuchukua hatua za kisheria dhidi ya Leeds United kutokana na kushindwa kumsajili mshambuliaji , Mfaransa Jean-Kevin Augustin. Leipzig imedai kuwa Leeds kwa mujibu wa mkataba ilikuwa inatakiwa kumsajili Augustin, ambaye alikuwa akicheza kwa mkopo katika klabu ya Elland Road msimu uliopita, kwa kitita cha pauni milioni 17.7 baada ya kwenda Ligi ya EPL.

Meneja wa timu ya Uingereza Gareth Southgate ameruhusiwa kurejea viwanjani kuendelea kuangalia wachezaji wa Ligi kuu baada ya kukaa nyumbani kwa muda mrefu kushughulikia mipango ya timu hiyo.

 

Tetesi za Soka Barani Ulaya.

Klabu ya Birmingham City iko kwenye mazungumzo na Ipswich Town kwa ajili ya kumnasa mshambuliaji Kayden Jackson. ofa ya Bournemouth ilikataliwa ilipomtaka mchezaji huyo, 26.

Newcastle wamemjumuisha kiungo mshambuliaji raia wa Ufaransa Florent Indalecio katika majaribio. Mchezaji huyo mwenye miaka 23 aliyekua akikipiga na Saint-Etienne kwa sasa hana klabu.


SHINDA NA MERIDIANBET!

Tengeneza pesa kidijitali kwa kubashiri mbio za farasi hapa Meridianbet! Chagua nani ashinde, unakusanya mkwanja.

 

Cheza Sasa.

43 Komentara

    Arsenal naona mnakuja kwa kasi sana katika usajili wenu

    Jibu

    Safii

    Jibu

    kwa usajili huu arsenal msimu huu watafanya vizuri

    Jibu

    Usajili unazidi kupamba moto huko kwenye vilabu

    Jibu

    Usajili naona umenoga kwa arsenal Mambo sio mabaya

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Usajili unaenda vizuri

    Jibu

    Tunasubiri michuano.

    Jibu

    Usajili uko poa

    Jibu

    Usajili uko vizuri sana tunasubiri mchuano@meridianbettz

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Asante kwa taarifa

    Jibu

    Ni habari nzuri za usajili ila Memphis Depay asiende Barcelona abaki zake ufaransa

    Jibu

    Usajili umepamba moto Arsenal nawaona wanavyo peta

    Jibu

    Asante kwa makala

    Jibu

    Man Chester wakazane sana kwenye isajiri bado kabic hawajapata kikosi kilicho kamilika

    Jibu

    Arsenal naona wako moto sana kwenye usajili#Meridianbettz

    Jibu

    Habar njema na asa kwa usajil

    Jibu

    Safii

    Jibu

    Vilabu vyote naona vinajitahidi kusajili wachezaji kwa kasi sana

    Jibu

    Arenal wazee wa kuchungulia pesa sijui kama wataweza kufanya usajili tena

    Jibu

    Habari nzuri za usajili na Vilabu vinajitahidi kusajiri sana ngoja tuone

    Jibu

    Tunasubulu michuano#meridianbettz

    Jibu

    Imekaa poa sana 👍

    Jibu

    Arsenal hawataki masihara kwenye usajili

    Jibu

    Usajili upo vizuri

    Jibu

    Arsenal wamejipanga sana mambo yatakua mazuri

    Jibu

    Usajili mzr

    Jibu

    mambo ni moto na meridianbet

    Jibu

    Mambo mazur

    Jibu

    Usajilii uko poa sana

    Jibu

    Taalifa nzur za usajir

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Nice.

    Jibu

    Arenal wazee wa kuchungulia pesa sijui kama wataweza kufanya usajili tena

    Jibu

    Nice update

    Jibu

    Safi afya kwanza mengine baadae!!

    Jibu

    everton wakimchukua uyu kiungo kutoka chelsea watakuwa wamefanya jambo jema sana kijana yupo makini

    Jibu

    Ipo poa sanaa

    Jibu

    Hot news

    Jibu

    Balaa ulaya

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.