Tetesi za Soka Barani Ulaya.


Tetesi zinasema mshambuliaji wa zamani wa Manchester City na Liverpool Mario Balotelli amefanya mazungumzo na timu ya Championi ya Barnsley. Muitalia huyo mwenye umri wa miaka 30 , yuko huru baada ya mkataba wake na Bresica kusitishwa kwa kutohudhuria mazoezi.

Chelsea wanataka kusaini mkataba na kiungo wa Borussia Dortmund na England Jude Bellingham, mwenye umri wa miaka 17 badala ya kiungo wa kati wa West Ham Declan Rice, 21.

Tetesi zinasema Meneja Pep Guardiola bado hajaamua kuhusu hali yake ya baadaye katika Manchester City. Mkataba wake unaisha msimu huu.

 

Tetesi za Soka Barani Ulaya.

Leicester wanamfuatilia kwa karibu kiungo wa safu ya nyuma -kushoto Mreno Nuno Mendes, 18, ambaye anakipengele cha kumnunua cha pauni milioni 40 katika mkataba wake na Sporting Lisbon.

Kiungo wa kati wa zamani wa Juventus midfielder Claudio Marchiso amemtaka mchezaji wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba, 27, arejee katika klabu hiyo ya Italia.

United watapatia kipaumbele mauzo ya wachezaji mwezi wa Januari huku mlinzi wa England Phil Jones, 28, na Waagerntina mlinda lango Sergio Romero, 33, na beki Marcos Rojo,30, wakiwa na uwezekano mkubwa wa kuondoka katika klabu hiyo.

Tetesi zinasema mazungumzo ya mkataba wa Wolves na winga Adama Traore yamekwama kwasababu Muhispania huyo hafurahii muda anaopewa kucheza gemu.

Tetesi zinasema West Ham wamepewa ofa ya kusaini mkataba na mshambuliaji wa Real Madrid Muhispania Mariano Diaz, 27.

 

Tetesi za Soka Barani Ulaya.

Arsenal wanaangalia uwezekano wa kufanya mkataba wa kubadilishana wachezaji na Inter Milan ambao utamuwezesha Mdenmark na mlinzi wa zamani wa Tottenham Christian Eriksen, 28, kujiunga na the Gunners na kiungo wa kati Mswiss Granit Xhaka, 28, kuhamia katika klabu hiyo ya Italia.

Tetesi zinasema Arsenal wako katika mazungumzo ya kumuuza beki Mfaransa William Saliba kwa mkopo msimu ujao.

Meneja wa zamani wa Chelsea Antonio Conte anasema alitaka kusaini mkataba na mlinzi wa Liverpool Virgil van Dijk na Romelu Lukaku wa Inter Milan wakati alipokuwa katika klabu hiyo.

 

Tetesi za Soka Barani Ulaya.

Mshambuliaji wa Chelsea na Ufaransa Olivier Giroud, 34, atakwenda mapumzikoni mwezi Januari kama muda wake wa kucheza hautaongezwa katika kipindi cha miezi ijayo .

Arsenal hawatamsaini Mitchel Bergkamp – mtoto wa kiume wa mchezaji wa zamani wa Gunners Dennis Bergkamp – licha ya kwamba Muholanzi huyo mwenye umri wa miaka 22 amekuwa akifanyiwa majaribio ya kimchezo kwa wiki moja katika klabu hiyo.


BASHIRI UKIWA MAHALI POPOTE!

Hauhitaji kuwaza linapokuja suala la ubashiri na odds kubwa. Bashiri na Meridianbet ukiwa popote ufurahie ushindi mkubwa katika michezo mbalimbali na hadi milioni 16 kwenye michezo ya kasino.

Meridianbet Beti Popote

INGIA MCHEZONI!

25 Komentara

    West hurm wasilaze damu kwenye hiyo ofaa

    Jibu

    balotelli sasa atafute timu atakayoweza kucheza mpaka kustaafu maana umri unaanza kumtupa mkono

    Jibu

    Kazi na umri

    Jibu

    Tetesi ziko poa na mambo yanazidi kunoga ila wachangamkiye hiyo ofa

    Jibu

    Ballotel ni bora ajirekebishe kinidhani hata kama haipendi timu hiyo inabidi aendane na sheria za michezo kupata haki yake lakini sio kimibavu la sivyo inawezekana akakosa sehemu ya kwenda kutokana na tabia yake

    Jibu

    Mpo vizuri kwa taarifa

    Jibu

    Asante kwa makala

    Jibu

    Nice update

    Jibu

    Meridianbet mpo vizuri update ya kibabe

    Jibu

    Ballotel mkorofi sana

    Jibu

    Makara mazuli

    Jibu

    Kumbe Balotel yupo

    Jibu

    Asantee kwa makala

    Jibu

    Asante kwa taarifa

    Jibu

    Gud news

    Jibu

    Barotel ni chezaji mzuri tu hila ndio hivyo tena hutukutu umezidi sizani kama kuana klabu yoyote ambayo hitataka sain yake

    Jibu

    Timu nyingi zinahusishwa kwa usajili lakini matokeo yake kimya

    Jibu

    Nice update

    Jibu

    Balotel kumbe duuh noma sana aache ukorofi

    Jibu

    Habari 🔥🔥

    Jibu

    kazi na umri

    Jibu

    Balotel bado anadai atakama wasema umeenda ila kipaji akipotei yupo vizuri Balotel nabado nguvu anazo wamsajili tuu apige kaz

    Jibu

    Good news

    Jibu

    Safi

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.