Kocha wa Aston Villa, Dean Smith anakusudia kukiimarisha kikosi chake katika safu ya ushambuliaji baada ya kufanikiwa kuepuka kushuka dara kutoka Premier League.
Katika kuhakikisha inafanikiwa katika hilo, wamekusudia kumsajili mshambuliaji wa Liverpool, raia wa Ubelgiji Divock Origi, 25.

Origi amefanikiwa kucheza jumla ya michezo 44 pekee ndani ya Liverpool msimu huu uliyomalizika, lakini mara zote amekuwa mtu wa kusugua benchi akiwapisha Mo Salah, Sadio Mane na Roberto Firmino wakianza.(Sun)
Mabingwa wa kombe la FA klabu ya Arsenal wanamlia rada beki wa kati raia wa Brazil, Diego Carlos huku Mikel Arteta akikusudia kukisuka upya kikosi chake kwaajili ya msimu ujao. (Telegraph)

Arsenal inatarajia kutoa ofa nono kwa mshambuliaji wake raia wa Gabon, Pierre-Emerick Aubameyang 31, wiki hii ya pauni milioni 250,000 kwa wiki katika makubaliano ya miaka mitatu kuendelea kusalia kwenye klabu hiyo. (Mirror)

Kocha wa Tottenham Jose Mourinho amepewa fursa ya kumsajili mshambuliaji wa Watford Troy Deeney, 32, kuchukua nafasi ya Harry Kane kwa muda. (Mail)
Liverpool imeitangulia Paris St-Germain katika kinyang’anyiro cha kutaka kumsajili Thiago Alcantara wa Bayern Munich na sasa hivi ina uwezekano mkubwa wa kumsajili kiungo wa kati wa Uhispania. (Mundo Deportivo, via talkSPORT)

Mtendaji Mkuu wa Manchester United Ed Woodward amefanya mazungumzo na wawakilishi wa mchezaji wa Lille Gabriel Magalhaes juu ya uhamisho wa mlinzi huyo wa Vrazil, 22. (RMC Sport, via Express)
Wakati huohuo, United inamatumaini ya kumtumia mlinzi Chris Smalling, 30, katika makubaliano ya mabadilishano na mlinzi wa Inter Milan, 25, raia wa Slovakia Milan Skriniar – lakini Roma inaendelea na machakato wake wa kumtafuta Mwingereza baada ya kuiridhisha timu hiyo alipokuwa kwa mkopo. (Star)
Tiketi yako ya kwanza kamwe haiwezi kupoteza ukiwa na Meridianbet. Unarudishiwa 100% ya Tiketi yako ya kwanza.


Gabriel
Habar njema sana 👍
Furahav
Aston villa amchukue tu origi.
Amiri Kayera
Habar nzur
Shafii
Tetesi zimekaa poa.
Venerose
Safi sana
Rehema
Bonge la makala
Caroline
Asante Sana meridianbet
Mwajumah
Habari nzuri
Adelta
Habari nzuri #meridianbettz
magdalena
aston villa pamoja na kufanya usajili wanatakiwa waongeze juhudi katika kufikia viwango bora kimpira
Dorophina
Aston villa msimu ujao inabidi waimarisha kikosi kiwe poa zaidi wasije wakashuka daraja
Ester jackson
Habari njema hizi kwawale wa mchezaji ambao wako benchi kusajiliwa kwao inawapa fursa ya kwenda kuonyesha kuwa nao walikuwa bora kuwepo uwanjani pale walipo kosa nafasi hizo
aisha
Hongera sana kocha wa Aston villa kwa kuimalisha kikosi chako ni jambo la maana sana ambalo umeliamua
warda
Hapo watakuwa wamefanya vizuri #Meridianbettz
Zeiyana
Jinsi gani arsenal walivyo samini huwepo wake aubameyang
felister
Aston villa inabidi wasijili msimu ujao ili kuimarisha kikosi zaidi
Njiku
Hii ya aston villa hii na mashaka na forwald wetu mbwana samatta kukosa namba au kutolewa kwa mkopo baada ya kuonyesha kiwango kibovu pale villa park akija orig kutoka liverpool
Tatu
Habari njema
Zuhura omary kindamba
Hakika hi ni Habali njema
Sadick
Thiago Alcantara amekuwa Lulu mara Man City,mara Liverpool na sasa nasikia PSG#meridianbettz
Khadija
Habari njema#meridianbettz
Issa
Aston villa kumchukua orig sidhan kama samata atakuwa na nafasi hapo
Frank
Hawa Arsenal hawa kama yangaa
Fatuma kasomo
Habar njema
Devotha
Good
Saupha mohamed
Good news
Hope mwaikuka
Imeeleweka hii
Ernest
Binafsi naliangalia hili deal la Divock Origi kama ni ishara nzuri kwa Origi kwani atapata muda mwingi wa kucheza tofauti na anavyopewa Liverpool
Lydia Emmanuel Magoti
Habari njema sana
David Pere
Zipo vizuri