Tetesi za Usajili Leo: Chelsea Mazungumzoni Kumnasa Countinho

Cheslea wanaripotiwa kuwa tayari wameanza mazungumzo na Barcelona juu ya Usajili wa Philippe Countinho. Countinho anatarajiwa kuondoka Barcelona moja kwa moja mwisho wa msimu huu wakati kwa sasa akiwa Bayern Munich kwa mkopo. Katika kusubiria kurejea kwa Ligi Kuu Uingereza, staa huyu anatarajia kurejea tena Uingereza.

Kwingineko katika usajili

Real Madrid wanajiandaa kufanya mabadiliko makubwa wakati ripoti zikitaja kuwa raisi Florentino Perez anataka kufanya mabadiliko kikosini huku James Rodriguez, Gareth Bale na wachezaji wengine 14 waliopo klabu zingine kwa mkopo wakionekana kuwa changamoto.

Newcastle wao wanaripotiwa kuw wapo karibu kufanya mabadiliko mapya wakihusishwa na meneja mpya klabuni hapo. The Mirror wame chapisha kuwa aliyekuwa bosi wa Tottenhma, Mauricio Pochettino ni mmoja kati ya wanaowindwa.

Klabu ya Inter Milan inatarajia kumuongezea mkataba Ashley Young kutokana na jitihada zake klabuni hapo. Kwa mujibu wa The Guardian, Inter wanatarajia kumuongeza mkataba wa mwaka mmoja zaidi.

Diogo Dalot anaweza akaondoka klabuni Manchester United. kwa mujibu wa The Sun, united wapo tayari kuanza kupokea ofa kwa staa huyu mwenye miaka 21 aliyefika klabuni hapo Juni 2018.

Taarifa nzuri kwa Roma ni kuwa Chris Smalling wa Man United na Henrick Mkhitaryan wa Arsenal wataendelea kusalia klabuni hapo.

2 Komentara

    Fundi mmoja.

    Jibu

    Vizur

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.