TFF - Morrison ni Mali ya Simba

Bernard Morrison, winga mpya wa Klabu ya Simba rasmi atakipiga kwenye klabu hiyo baada ya Shirikisho la Soka Tanzania kumtambulisha kwamba ni mchezaji wa timu hiyo.

Agosti 30 kwenye kilele cha Wiki ya Mwananchi Yanga ilimtambuisha Morrison kuwa mmoja kati ya wachezaji wake 28 kwa kueleza kuwa mchezaji huyo kesi yake ipo Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Masuala ya Wachezaji,(Cas).

Mchezaji huyo pia Agosti 22 kilele cha Simba Day alitambulishwa kuwa mchezaji wa Simba na Agosti 30 jambo lililomfanya awe mchezaji pekee aliyetambulisha mara mbili ndani ya Uwanja Mkapa.

Morrison aliyekuwa na mvutano na mabosi wake hao wa zamani, alitajwa kwenye kilele cha Wiki ya Mwananchi kama mchezaji wa Yanga, akiwa jijini Arusha kukinukisha kwenye mechi ya Ngao ya Jamii ya timu yake mpya ya Simba iliyoishinda Namungo kwa mabao 2-0.

Lakini mashabiki wakiwa bado hawaamini kama nyota huyo aliyewapa raha msimu uiliopita kwa kuwatungua Simba katika mechi ya marudiano ya Ligi Kuu Bara, atasalia kikosini mwao, katika orodha ya usajili mpya ya TFF kwa msimu ujao jina lake limetokezea Simba kuonyesha ni mali yao rasmi sasa.

Ofisa habari wa TFF, Cliford Ndimbo, amesema kilichomfanya Morrison awe kwenye orodha ya Simba badala ya ile ya Yanga ni kwa kuzingatia maamuzi ya Kamati  ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji iliyomtambulisha kama mchezaji huru baada ya kusikiliza kesi iliyomhusisha Mghana huyo na Yanga.


SHINDA NA HI LO

Sasa hii ni rahisi zaidi kupata USHINDI! Unatabiri karata ipi ipo chini au juu, kisha unakusanya mkwanja wako.

Cheza sasa

37 Komentara

    Yote heri mana safari bado inaendelea

    Jibu

    Merrison wakawaida tu simba waache habari za Morrison wazungunze na habari za kagere kumpiga kocha kichwa na alivyo komaa sijui hana ali gani uyo kocha

    Jibu

    Morrison hatukutaki yanga.kwanza ww ndo ulisababisha tukafungwa nne.msaliti mkubwa wewe

    Jibu

    Wamuache morison aende anapopahitaji..morison ni wa simba tuu huko yanga hana anachokiitaji

    Jibu

    utopolo wanatapatapa na kujipa matumaini ya kuwa morissoni atarudi kwao waache tu kujipa matumaini ayo

    Jibu

    Maamuzi Ni yake mwenyewe @meridianbettz

    Jibu

    Morrison yuda haende tu huko simba sisi hata hatumuhitaji tena

    Jibu

    Maamuzi ni yake mwenyewe

    Jibu

    Morrison ni mchezaji mzur sana karibu simba ila ule ujeuri wa zaman ulipokua yanga uwache ukouko kwa utopolo#Meridianbettz

    Jibu

    aende tu hatumtaki wala nini

    Jibu

    Morrison ni wa Simba tu

    Jibu

    Hapa hatutaki tena kusikia fyokofyoko za wazee wa kikapu aka Utopolo Fc, wajipange kivingine pia iwe fundisho kwa viongozi wa club hapa nchini kwenye kwenye Janja janja kuhusu mikataba ya wachezaji maana ilikuwa Aibu kubwa kwa Mchezaji mkubwa kama Morrison kupata kashfa kama hii wakati yeye ni Professional na anaelewa kazi yake, Viongozi wa Yanga na vilabu vingine vyote hapa Nchini Tanzania kuna kitu cha kujifunza Hapa.

    Jibu

    Yanga inamatatizo sana badala wajipange kwa ajili ya msimu ujao wao wanapoteza mda kwa mchezaji mmoja kama Morrison

    Jibu

    Vizuri Sana Morrison kuwa halari yasimba iyo ainaubishi mbona inaeleweka Kama Morrison Ni wasimba

    Jibu

    Ahsant meridian kwa taarifa

    Jibu

    Habari njema kwa wana msimbazi.

    Jibu

    Hongera sana morrison

    Jibu

    Issue ya Morrison imeonyesha namna ambazo tunaendesha mambo yetu bila kufuata utaratibu#meridianbettz

    Jibu

    Ndioooo ni mali ya mabingwa

    Jibu

    Karibu simba damu morrison hila umejua kuwakausha mashabiki koo#meridianbettz

    Jibu

    Tff kama wanaleta ushabik kwenye hili swala la morrison wasubir wazee wa utopolo maamuz ya fifa kuhusu hili swala

    Jibu

    Wanayanga lazima watoke mapovu,ila Morrison yupo unyamani atakiwasha balaa!!!

    Jibu

    Bora wanna yanga watulie tumechoka na madai yao

    Jibu

    Karibu sana

    Jibu

    vizuri na ubora wake umeonekana

    Jibu

    Ishu ya morrison itasumbua sana tff isimamie kwenye haki si kutoa maamuz sabab ya ushabik

    Jibu

    Karibu sanaaa

    Jibu

    Kesi hii imeshikiliwa sana kiushabiki kuweni wapole hadi itakapo tolewa uamuzi

    Jibu

    Karibu sana

    Jibu

    Morrison ni mchezaji mzuri Sana

    Jibu

    Bm3 sheria imefuata mkondo wake

    Jibu

    Yanga wanajua Ila wanawaongopea mashabiki zao

    Jibu

    Morrison hatukutaki yanga.kwanza ww ndo ulisababisha tukafungwa nne.msaliti mkubwa wewe

    Jibu

    Wana yanga mmesikia iyoo

    Jibu

    Hadi raha

    Jibu

    Simba wa wanajifariji

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.