Timu za Ligi za Tanzania Zijiongeze Katika Swala la Udhamini

Ni namna gani timu ya ligi kuu au daraja la kwanza au timu yoyote inaweza kuji-brand na kuvutia makampuni mbalimbali kuwekeza kwenye klabu hiyo?. Angetile Osiah kupitia kipindi cha redio cha Sport Extra ya Clouds fm jana alitoa darasa huru.

Timu zinatakiwa kujiweka kisasa na kuajiri wataalam wa masoko ili kuwatafutia wadhamini pamoja na kuishauri TFF kuwaandaa wataalam wa masoko. Timu zetu inafika mahali zinahangaika kutafuta wadhamini ili kukidhi mahitaji yao, wakati akiwa TFF aliwahi kuwaita viongozi wa vilabu kwa ajili ya kuzungumza masuala ya marketing lakini hawakuwa tayari sana pengine walidharau kwa sababu wanafikiri wapo karibu na wafanyabiashara wakubwa wanadhani ule uhusiano wao utaketa wadhamini.

Proposal nzuri ndio zinaweza zikafanya wadhamini watamanibkuingia kwenye klabu fulani wakijua kujihusisha na klabu hiyo watawafikia watu wanaowalenga. Kwa hiyo vilabu vinatakiwa kufanya mpango mkakati kwa ajili ya kuvuta wadhamini na hiyo inafanywa kwa kutengeneza program ambayo inamuonesha mdhamini ananufaika vipi na uwekezaji wake kwako. Kwa mfano kuwa na activities yungi ambazo zitamfanya aone ataweza kujitangaza kupitia hizo activities.

Kwa mfano usajili wa timu. Kwa mfano mchezaji kama Paul Pogba kwenda Manchester United nyuma ya dili hili ilikuwepo kampuni ya Adidas ambayo ilikuwa inajua Man United ni maarufu duniani lakini inatatizo la vijana kwenye mitandao ya kijamii kwa hiyo Pogba alikuwa anatarajiwa kuwavuta vijana wengi kwenye mitandao.

Siku ambayo Pogba anatambulishwa kilifanyika kitu kinaitwa marketing division, walitengeneza video ya dakika moja na kuipeleka mitandaoni na ikapata views wengi sana.

Kwa hiyo ni kuangalia kampuni zetu zinamahitaji gani na vilabu vyetu vifanye nini ili kugusa mahitaji ya wateja wao. Kumtaji mdhamini ni jambo moja lakini haitoshi kumpa thamani, unatakiwa kumhusisha kwenye activities zako za kila siku lakini kama hauna mdhamini hapati anachotarajia.

Tatizo jingine kwa vilabu vyetu ni kuwatunza hawa wadhamini. Unakuta mdhamini mmoja anachukua nafasi kubwa kwenye klabu yenye mdhamini zaidi ya mmoja kiasi cha mdhamini kushika activities zinazopaswa kufanywa na watendaji matokeo yake anapata milage kubwa kuliko wengine

9 Komentara

    Elimu ndogo ya viongozi na ubinafsi ndio chanzo cha yote

    Jibu

    Kwel kabisa

    Jibu

    daah nshida yn

    Jibu

    Tatizo wadhamin hawapat faida katika timu ndogo

    Jibu

    Nii kweli

    Jibu

    Ni kweli kabisa

    Jibu

    Ni kweli

    Jibu

    Kweli kabisa iyo

    Jibu

    Ni sawa kabisah

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.