Tuchel: Natumai Carlo Ancelotti Atakuwepo kwenye Benchi

Kocha wa klabu ya Chelsea Thomas Tuchel anatumai kuwa kocha wa klabu ya  Real Madrid Carlo Ancelotti atafanikiwa kuwepo kwenye benchi la timu hiyo kwenye mchezo wao wa kwanza wa robo fainali ya ligi ya mabingwa ulaya siku ya jumatano.

Kocha wa Real Madrid  hajasafiri na timu yake kwenda kwenye jiji la London leo jumanne kutokana na kutokumaliza vupimo vyake vya Uviko-19.

Tuchel

“Mara zote ni vizuri na bora kuwepo kwenye benchi lako  na kutoa hamasa ya moja kwa moja,” alisema Tuchel.

“Nina taarifa kuwa atawasili jioni ya leo.”

Carlo Ancelotti amekosa mchezo wa Real Madrid dhidi ya Celta Vigokwenye ligi kuu ya Hispania La liga, ambao madrid walifanikiwa kushinda kwa goli 2-1, kwa sababu alikutwa na maambukizi ya Uviko-19 baada ya kufanyiwa vipimo tarehe 30 March.


 

3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!

Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.

Kubeti Poa - Bonasi Kubwa

Jisajili sasa

Acha ujumbe