Lakers Yatupwa Nje Kunako NBA.

Safari ya matokeo mabaya kunako NBA msimu huu, imetamatika kwa LA Lakers kutupwa nje ya mashindano hayo kwa mwaka huu.

Lakers wamejikuta wakimaliza mzunguko wa kwanza wakiwa nafasi ya 11 kwenye msimamo wa Western Conference. Kipigo dhidi ya Phoenix Suns ni kipigo cha 7 mfululizo kwa vigogo wa jiji la Los Angeles.

Kwa mujibu wa sheria na muundo wa NBA, timu 7 zinafuzu hatua ya mtoano. Ambapo, nafasi ya 1-5 zinafuzu moja kwa moja, nafasi 2 kati ya 7 (6 na 7) zinajazwa na washindi wawili watakaofanikiwa kuvuka hatua ya Play-in ambayo inazikutanisha timu zilizomaliza kwenye nafasi ya 7-10.

Lakers

Pamoja na uwepo na nafasi hizo, bado LA Lakers wanakua nje ya hesabu za msimu huu baada ya kumaliza katika nafasi ya 11 kunako msimamo wa NBA msimu huu.

Hii inakua ni mara ya 4 kati ya miaka 19 ambayo, LeBron James anashindwa kufuzu hatua za mbele kwenye maisha yake yote ya kucheza ligi ya NBA. Hali sio shwari kule Staple Centre baada ya kushindwa kutetea ubingwa wao kwa misimu miwili mfululizo.


3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!

Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.

Kubeti Poa - Bonasi Kubwa

Jisajili sasa

Acha ujumbe