Jadon Sancho, 20, ametajwa kuwa anataka kurejea Ligi Kuu ya Uingereza baada ya kuondoka huko mwaka 2017. Alitokea Manchester City kwenda kukipiga Bundesliga akiwa na Borrusia Dortmund hadi leo. Kwa msimu wa 2019/2020 amecheka na nyavu mara 14 na kutoa asisti 15.
Tangia aondoke Manchester City kwenda Ujerumani ni kama alipiga hatua kubwa zaidi na uwezo wake umewavutia klabu nyingi Ulaya, zikiwepo kadhaa kutoka EPL, na mpaka sasa mipango ya nani apate nani amkose inachezeshwa mezani! Hapa tunagusa kidogo klabu zinazomfukuzia kiasi cha kufanya usajili wake uwe kama gombania goli, atakayempata ndiye huyo mshindi!

Manchester United
Manchester United wanataka kumsajiuli Jadon Sancho dirisha la usajili litakapofunguliwa. Wakati huo bosi Ed Woodward ameonya kuwa mambo hayatakuwa kama yalivyozoeleka kwenye uhamisho wa sasa.
Lakini ukweli ni kuwa United wanataka kufanya lolote linalowezekana kuboresha safu ya ushambuliaji kuelekea msimu ujao na Jadon Sancho ni moja ya karata wasiyotaka kuipoteza.
Chelsea
Bila shaka, hakuna kitu mashabiki wa Chelsea kitawasuuza mioyo yao kama kumuona Jadon Sancho ametua klabuni hapo msimu huu wa joto! Chelsea pia wamehusishwa kuingia kwenye kinyanga’anyiro cha kuinasa sahihi ya kinda huyu kutoka Dortmund.
Frank Lampard na kikosi wanajitahidi kuona namna bora ya kumnasa. Kinda huytu ameenda kuwa bora zaidi ya baadhi ya wachezaji wa Chelsea ambao amewahi kucheza nao, sasa wanataka aongeze nguvu kikosini.
Liverpool
Liverpool wamekuwa wakihusishwa na Jadon Sancho, beki wa Liverpool Alexander Anorld alinukuliwa akisema kuwa itakuwa poa sana kama staa huyu akitimba kwa majogoo, anaamini kikosi chao kitakuwa bora zaidi na kwake binafsi itakuwa poa zaidi.
Sancho ameweza kumjibu Anold kupitia ukurasa wake wa Instagram, na huenda akawa amewaacha na matumaini Liverpool baada ya kuchapisha macho mara 4 alipokuwa anahusishwa na kuhamia Liverpool na Alexander Anorld ikiwa ni ishara kuwaa anaweza kuwa anafahamu jitihada za chini ya kapeti.
Sio EPL tu!
Hata hivyo sio vilabu vya EPL tu vinavyowinda sahihi ya Jadon Sancho. Barcelona pia wametajwa kuwa wanaisaka sahihi yake na anaweza kuwa mbadala wa Neymar klabuni hapo.


Theckla
Kizuri kinajiuza Mana jadon Sancho ni mchezaji ambaye anaonyesha jitihada za Hali ya juu pindi anapokuwa uwanjani
Tatu
Mchezaji mzuri sana
Furahav
Nenda man u sancho.
Samira
Aende man united😋
Rehema
Mchezaji hatarii hatarii
Lydia Emmanuel Magoti
Namkubali mchezaji mzuri nayupo vizuri azidi kulisongesha kabambe
Gabriel
Uje England tu
Mwajama
Bora aje man u
John mwakalosi
Huyu bora abaki huko ujeramani au aende spain tu asirudi uingereza
Mariam
Yupo vizur
Mwanahamisi
Bora aje man u