Manchester United waliamua kumuuza Romelu Lukaku kwenda Inter Milan kwa £74m. Uamuzi ambao baadhi ya wadau walishangaa na kuhisi ilikuwa ni makosa.
Moja ya watu ambao hawakuwaelewa United kwa nini waliamua kumuuza Lukaku, ambaye sasa ameendelea kung’ara Serie A ni Troy Deeney.
Nyota huyu aliondoka United msimu wa Joto wa 2019 kuungana na Inter Milan kwa ada iliyotajwa kuwa €74m baada ya kutumikia misimu miwili pale Old Trafford.
Nyota huyu alipokuwa United aliangaziwa sana na wakosoaji, lakini bado alifanya kazi nzuri akiondoka na magoli 42 katika mechi zake 96 alizocheza.

Nyota huyu, amekuwa na stori nyingine na kuwa bora tangia alipoondoka United, akiwa na magoli 41 katika mechi 57 za michuano yote kwa Inter Milan, magoli 34 akiwa ameyapata msimu uliopita.
Lukaku pia amefanya vizuri katika ngazi ya Mataifa akiwa na timu yake ya taifa ya Ubelgiji. Ameshinda magoli 24 katika mechi 23. Alitoa mchango mzuri wa asisti katika mechi ya Jumapili dhidi ya Uingereza waliyoibuka na ushindi.
Troy Deeney anasema kuwa Lukaku hakuwa na rekodi mbaya kiasi cha United kuona ulazima wa kutemana naye. Anaamini United wana changamoto ya jumla ya ushambuliaji.
Troy Deeney Juu ya Lukaku
“Yuko vizuri sana, na wakati wote niliona ulikuwa uamuzi mgeni sana United kuamua kuachana naye.”
“Tangia ameenda Italia unaweza kuona upande wa ufundi wake na upande wa kocha, amekuwa bora maradufu. Ana kitu cha kuthibitisha.”
Hauhitaji kuwaza linapokuja suala la ubashiri na odds kubwa. Bashiri na Meridianbet ukiwa popote ufurahie ushindi mkubwa katika michezo mbalimbali na hadi milioni 16 kwenye michezo ya kasino.



Adelta
Manchester united kwa sasa sijui wanakwama wapi?
magdalena
tatizo la united viongozi wake wanafanya mambo kwa kukulupuka sana awafikirii mbele
Elika
Man u hamna kitu hapo
Sauda
Lukaku fundi
Ester jackson
Wanajutia hasaivi walimuona lukaku ameshuka kiwango kwenye mechi kadhaa wakaamua kumuuza bida yakumpa nafasi sasa hasaivi wanajutia inter Milan wanafurahia kutesa kwa zamu
Angelina
Man u hawajatuliza akili
Gabriel
Lukaku jembe
Rahma
Lukaku Yuko vizuli
Carolyn
Kweli kabisa walifanya makosa
Lydia Emmanuel Magoti
Nikweli Man U Wana suasua tena Lukaku akutakiwa kuzwa kwasababu kila mtu anajina kwenye krabu ana mamuzi ndio kilicho tokea hicho kwaio wasiongee tena kumkumbuka lukaku
Hopemwaikuka
Walikosea sanaa
Ernest
Mzimu wa Lukaku utawasaka Man U tuu
zeiyana
Man u aliofia mri wake lukaku hawakuangalia uwezo wake sasa wanajutia mahamuzi yao
Saupha mohamed
Kweli kabsa man u awaeleweki
Janeflora malisa
Mtian
aisha
Lukaku ndio alikua mtu ambae anaibeba sana timu
Tatu
Hichi kitu nilijua tu man u kama wangejutia kwani wamemuuza jembe lukaku
Povel
Kivuli cha lukaku bado kina watafuna manchester united
Issa
Usajil wa lukaku kwa man ulikua mzur ila wakurugenz hawakumuamin sana
Fatina mfingi
Ni kweli ila hawakufukiria kwa Makin walikurupuk man U kwa kweli!!
Mwajumah
Man u watamtafuta lukaku na watajutia maamuzi yao
Sabrina
Tatizo la man u wanakurupukaga