Mchezaji wa Villarreal, Gerard moreno amekuwa tageti ya timu ya Manchester United pamoja na Barcelona ambao wote wanataka huduma yake, taarifa kutoka jarida la Fichajes zinasema hivyo.

Katika michezo 46 aliyocheza na Villarreal, Moreno alifanikisha kufunga magoli 30, kitu kilichomfanya kuwa miongoni mwa mastraika bora ulaya katika kampeni ya sasa. Uchezaji wa Moreno umeshangaza watu wengi na imesababisha klabu ya Barcelona na Manchester United kutaka saini yake.
Moreno
Moreno akishangilia goli katika mechi ya fainali ya Europa

Mchezaji huyu wa miaka 29, anawindwa na klabu hizi na inategemewa mwenye bahati. Bado haijatajwa Villarreal watahitaji kiasi gani lakini kwa uwezo alionesha msimu huu, bila shaka atakuwa na thamani kubwa sana.

Barcelona wamesajili Sergio Aguero hivi karibuni lakini Gerard atakuwa ongezo lingine muhimu katika kikosi hicho cha Barcelona. Kwa upande wa Manchester United, kuongeza kwa mkataba kwa Cavani ni muhimu lakini kutokana na umri wake, hawezi kucheza kila mechi na Gerard atakuwa muhimu sana klabuni hapo.


MAANA KAMILI YA USHINDI KATIKA KASINO ZA MERIDIANBETI NI PAMOJA NA MCHEZO WA PANDA PANDA.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Panda Panda na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

Gomes, Gomes : Sitafanya Usajili wa Kutisha., Meridianbet

CHEZA HAPA

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa