Virgil Van Dijk, Fabinho na Curtis Jones leo wameonekana kwenye uwanja wa mazoezi wakifanya mazoezi na wachezaji wengine baada ya muda kujitenga kutokana na uviko-19 kuisha
Virgil Van Dijk, Fabinho na Curtis mchezo wao wa mwisho kuichezea timu ya Liverpool ni kwenye mchezo ambao Liverpool ilishinda 3-1 dhidi Newcastle Disemba 16, kabla ya wachezaji hao kukutwa na maambukizi ya uviko-19.

Kuahirishwa kwa mchezo kati ya Liverpool dhidi ya Leeds siku ya “Boxing Day” kutawapa nafasi ya kuweza kufanya mazoezi pamoja na wachezaji wengine kwa muda mrefu kidogo kabla ya kusafiri kwenda kucheza na Leicester City Disemba 28.
Kiungo Thiago Alcantara hatarajiwi kuwepo kwenye kikosi kitakachosafiri kwenda Leicester, baada ya kuendelea kujitenga kutokana na muda wake wa maangalizi kutokwisha, pia Livepool watamkosa beki wa kushoto Andy Robertson kutokana na kuendelea kuitumikia adhabu yake ya kadi nyekundu.
Nani hapendi kuwa bingwa na kujishindia mkwanja wa kusahato kuelekea katika sikukuu wiki hii. Mchezo wa Ocean Call kutoka kasino maridhawa za meridianbettz unakupa kila sababu ya kuifanya siku kuu yako kuwa ya kuvutia zaidi.


