Luka Modric amekuwa mchezaji wa kihistoria baada ya kutwaa tuzo ya Ballon d’Or ambayo haihusishi uwepo wa Messi na Ronaldo kwa miaka ya hivi karibuni. Mchezaji huyo ametwaa tuzo hiyo baada ya kupitia kipindi kikubwa cha mafanikio makubwa kisoka. Mafanikio hayo ndiyo yaliyochangia kumuweka kwenye ramani akiwapiku wakongwe wa muda wote, akiwa amevunja historia ya mwaka 2017.
Kaka alikuwa ni mchezaji pekee aliyeshinda tuzo hiyo kwa mara ya mwisho kabla ya ujio wa Ronaldo na Messi siku za usoni. Upinzani wa wawili hao umedumu kwa kipindi kirefu sana kitu ambacho kiliwafanya kuwa wanasoka walioonesha upinzani mkubwa sana kisoka ikilinganishwa na miaka mingine ya utoaji tuzo hizo.
Sio mataji hayo aliyoyapa nyota huyo mwenye miaka 33 akiwa na Madrid yamemfanya ashinde tuzo hiyo bali kuna mengine mengi aliyoyafanya na timu yake ya taifa na yamemfanya aibuke kidedea kwenye tuzo hizo kwa sababu aliisaidia timu yake ya taifa ya Croatia kufika hatua ya fainali kwenye kombe la dunia.

Japo tuzo yake ilipingwa na wengi kwamba mchezaji huyo hakustahili kuipokea na haikuwa halali yake lakini 2018 ukawa ni mwaka wa mabadiliko katika historia ya soka kutokana na kushuhudia mchezaji huyo akiandika historia kwenye ulimwengu huu wa soka kwa miaka ya karibuni.
Kupitia hilo inaudhihirishia ulimwengu kwamba sio wafungaji pekee wanaweza kuitwaa tuzo hiyo bali pia hata wachezaji wengine kama walinzi, magolikipa na viungo wana uwezekano mkubwa wa kuitwaa tuzo hiyo na kufanya vizuri zaidi jambo ambalo kwa kipindi cha nyuma halikuwa la kawaida sana.
Mbali na Modric kuna viungo wengine wanahitaji kutambulika sana kutokana na mchango wao wanaozidi kuuonesha kwenye vikosi vyao. Mengi yanafanywa na wachezaji hao lakini bado hayapewi ile hali ya kutambulika sana kama ilivyo kwa wale wengine. Mbali na hao kuna wengine kama David Silva, Kevin De Bruyne na Sergio Busquets.
Zifuatazo sasa ni takwimu za viungo wengine wanaofanya vizuri kwenye historia ya soka: Luka Modric (Real Madrid na Croatia), Toni Kroos (Real Madrid na Germany), David Silva (Manchester City na Spain), Kevin De Bruyne (Manchester City na Belgium), Miralem Pjanic (Juventus na Bosnia), Sergio Busquets (Barcelona na Spain). Hao ni baadhi tu lakini wapo wengine pia kama:
Paul Pogba (Manchester United na France), Bernardo Silva (Manchester City na Portugal) na Thiago Alcantara (Bayern Munich na Spain). Ni vigumu kukubaliana na takwimu kama hizi lakini kutokana takwimu za wachezaji hao zinawafanya wakae katika nafasi hiyo nyeti na muhimu na yenye ushindani mkubwa sana.


Povel
Gud news
Issa
Safi modrick