Afrika ni miongoni mwa bara linaloongoza kuwa na wachezaji wenye uwezo mkubwa na historia ya kipekee ambao wanafanya vizuri ndani na nje ya mataifa yao ya asili. Ni bara lenye historia pia ya kutoa wachezaji waliojenga historia kubwa yenye heshima duniani kutokana na kuweka kwenye kalenda wachezaji waliowapa changamoto ya kisoka wachezaji wengine kutoka Ulaya.
Bila chombo imara kinachosimamia maslahi na viwango imara vya wachezaji hao yamkini wasingekuwepo wachezaji ambao wameonesha uhai wa soka katika bara hili. Sio hivyo tu, pia utambuzi wa kuunganisha Afrika na nchi nyingine kupitia soka imesaidia sana kutambua vipaji mbalimbali vya wachezaji ambao wamepata nafasi kwenye vikosi vya nchi tofauti tofauti.
Kwa huku Afrika wenyeji wanaposikia habari za CAF wanafananisha mashindano hayo ambayo huandaliwa na shirikisho hilo kama yale ya Ulaya yanayoitwa UEFA. Haya ndiyo mashindano yanayoheshimiwa sana Afrika na kila klabu inayofikia hatua fulani kwenye mashindano hayo hupata heshima kubwa sana na kuonekana ni klabu yenye historia fulani.
Klabu nyingi za ukanda wa Afrika Mashariki zimeonekana kutofanya vizuri sana ndani ya mashindano haya kiasi kwamba hushiriki na kuishia nafasi za chini kabisa ambazo mara nyingi hutambulika kama nafasi za klabu zinazosindikiza klabu zenye nafasi kubwa kuweza kufika pale zinapotaka kufikia.

Katika miaka ya 1972 na 1991 baadhi ya klabu kutoka Afrika Mashariki zilionesha ukomavu na kufanikiwa kufanya vizuri sana japo hazikufika nafasi za juu sana. Miongoni mwa klabu hizo ni zile baadhi kutoka Uganda, AS Vita na Simba FC ambao walionesha mapinduzi kwenye kombe hilo kwa kujisogeza hadi hatua fulani inayoridhisha.
Baadhi ya klabu nyingine zilizowahi kufanya vizuri na zinaendelea kufanya vizuri ni Hafia ambayo iliwika sana miaka ya 1970 kwa kunyanyua ndoo tatu lakini kwa sasa hawajaonesha makali yao. Miamba hao wa Guinea walisumbua sana kwenye soka kutokana na makombe waliyonyanyua na aina ya kiwango walichokuwanacho.
Klabu nyingine zenye historia inayofanana na hiyo kwa kunyanyua vikombe vitatu ni wababe wa soka wa Morocco, Raja Casablanca ambao waliweza kufikia hatua hiyo; wengine ni wababe wa soka Cameroon, Canon Yaoundé nao waliweza kufikia hatua hiyo lakini tangu kipindi hicho hawajaweza kugusa tena hatua hiyo ya fainali. Wengine ni miamba wa soka Tunisia ambao nao walijenga historia yao kwa kunyanyua kombe hilo mara tatu ambao ni Sportive de Tunis na walijenga historia kwenye hilo.
Waliojenga historia kubwa zaidi kwenye michuano hiyo ni Zamalek ambao walinyanyua kikombe hicho mara tano na wengine ni TP Mazembe ambao bado wanasumbua kwenye michuano hiyo wakiwa mwaka 2015 walishinda taji hilo kwa kuwafunga USM Alger; pia waliweka heshima kwa kucheza na Inter Milan kwenye michuano ya FIFA Club World Cup. Mbali na hao kuna mbabe wao aliyenyanyua kombe hilo mara nyingi zaidi ambao ni Al Ahly kutoka Misri!


Furahav
Afrika kuna vipaji vingi sana.
Povel
Black lives matter
Chiku
Tanzania mpango mnzima