Mata: Vichapo Kitapima Morali ya United

Baada ya kupokea vichapo ikiwa ni pamoja na kichapo kilichowatoa kwenye Kombe la FA dhidi ya Wolves, Juan Mata anaamini kuwa huu ndiyo wakati wa majaribu kwa Manchester United ambao walishinda mechi nyingi mfululizo wakati Ole Gunnar akikianza kibarua chake cha mda kama meneja. Bado watakuwa na morali waliyoanza nayo?

United walikuwa wanajituma sana kama timu wakitahidi kundika ushindi wa kila gemu na gemu kadhaa kutoa sare kabla hawajapigwa na PSG, Arsenal na baadae Wolves. Hata hivyo, baada ya kupigwa na PSG kwenye ligi ya mabingwa Ulaya, walifurahisha kwa namna walivyorejea kwenye gemu ya pili na kuwachapa PSG wakiwa kwao, wakirudi na jeuri hiyo EPL wakakutana na kichapo Cha Arsenal, Wolves wakamalizia kuwaondoa kwenye njia ya FA Cup.

Juan anaamini huu ndio wakati ambao kikosi cha United inabidi kujitathimini na kurejea na mbinu mahususi ya kushinda kwenye mfululizo wa gemu ambazo zipo mbele yao kwa sasa. Gemu walizopoteza zinaweza kuwapa nguvu ya kuwa bora zaidi au kuwafanya watetereke zaidi kama watashindwa kurejea na kasi nyingine.

Hata hivyo, Ole Gunnar anasifika kwa hamasa yake kwa wachezaji na namna anavyoweza kwenda sawa. Na taarifa za chini ya kapeti zindai kuwa United wana mpango wa kumfanya meneja huyu kuwa meneja wa kudumu klabuni hapo.

Baada ya kipindi cha likizo ya kimtaifa, Juan anaamini kuwa watarejea na moto wa ajabu! Na kitakuwa ni kipindi muhimu zaidi kwao kwa msimu huu.

3 Komentara

    Sante meridianbet kwa habari nzuri

    Jibu

    Duuh poleni sana kwa kichapo maana mmepoa mmekua baridiiiiiiiiiiii😅😅😅😅😅

    Jibu

    Duh

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.