Kwa takwimu zinazoishi mpira wa miguu ni mchezo ambao unafuatiliwa sana duniani iwe ni kwa kuangaliwa au kuwa na mashabiki wengi. Ni mchezo ambao unafuatiliwa na zaidi ya watu milioni 265 na idadi hiyo inakua kadri siku zinavyosonga mbele. Leo tumekusogezea baadhi ya majina ya wachezaji ambayo kutatamka kwake kunahitaji jitihada kidogo ya ujifunzaji wake.
Cameron Borthwick-Jackson
Ni miongoni mwa majina marefu yanayopatikana duniani. Aliweza kujiunga na United tangu akiwa na umri wa miaka 6. Aliweza kubahatika kupandishwa katika kikosi cha timu ya kwanza kipindi cha Van Gaal lakini baada ya ujio wa Jose alimshusha na kumtoa kwa mkopo Wolves baadae Leeds na sasa yupo Scunthorpe.
Pierre-Emerick Aubameyang
Miongoni mwa wachezaji wanaoiwakilisha Afrika kimataifa. Raia huyo wa Gabon anakaa katika kundi la wachezaji wenye majina magumu na marefu kwenye soka, ambapo utamkaji wa jina lake mara nyingi unahitaji uelewa na umakini mkubwa. Ameweza kucheza katika klabu nyingi kubwa kama Arsenal na Dortmund.
Sotiris Papagiannopoulos
Mchezaji huyu raia wa Sweden pamoja na kwamba jina lake ni refu lakini kinachofurahisha zaidi ni ugumu uliopo katika kulitamka jina hilo. Mtangazaji mmoja wa Uingereza aliwahi kufurahisha umma baada ya kushindwa kulitaja jina hilo na kuamua kughuna kwa baadhi ya sehemu.
Mohamed Lamine Zemmamouche
Mchezaji raia wa Algeria ambaye jina lake kiuhakisia ni refu sana na kuna walakini wakati wa kulitaja. Ni chaguo la pili ndani ya kikosi cha Algeria japo hajapata wakati mwingi kuweza kukaa katikati ya milingoti miwili, lakini anakaa katika historia hiyo.
Jakub Błaszczykowski
Raia huyo wa Poland ni miongoni mwa wachezaji ambao majina yao yanahitaji uelewa mzuri wa asili ya taifa hilo. Ni jina ambalo sio rahisi kwa mtu kulitaja. Hata watangazaji wamekuwa wakipata ugumu kulitaja jina hilo zaidi wamelifupisha na kumwita ‘Kuba’ ili kurahisisha utamkaji.
Jan Vennegoor of Hesselink
Mchezaji huyo wa zamani wa Celtic na mshambuliaji wa Hull, jina lake ni miongoni mwa majina yanayofurahisha sana katika karne hii kutokana na urefu wake na baadhi ya sehemu kuwa na ugumu kuzitamka. Jina lake lina muunganiko wa familia zake zote mbili na kulifanya kuwa refu sana hata kulitamka; na wakati mwingine huwapa ugumu watangazaji.


Furahav
Mmh hatari.
Ester jackson
Nakweli wana majina magumu sana
farida ahmadi
Duh nouma hiyo habari nzuri Sana kwetu mashabiki
Zeiyana
Asante kwa makala