Umri ni suala ambalo hakuna kiumbe anaweza kuzuiana nao ukiwa tayari umefika hasa pale unapokuzuia kufanya kitu fulani ambacho wewe ungependelea kuendelea kukifanya lakini kutokana na harakati hizo kuwa ngumu unaamua tu kuacha wakati huo uweze kupita na wewe kuipokea hatua hiyo katika mazingira ya urafiki tu.
Wapo wachezaji wanaopenda kuendelea kucheza soka hata kwa maisha yao yote bila kujalisha suala la umri kwao; lakini ni jambo ambalo kwa kawaida linakuwa gumu kuendana nalo kutokana na kile kinachoitwa wakati. Hata kiwango cha mchezaji kwa wakati huo katika hali ya kawaida huweza kushuka kutokana na hilo.
Mshambuliaji hatari wa pembeni wa klabu ya Bayern Munich na mkongwe wa klabu hiyo, Arjen Robben aliweza kueleza uhalisia wake na kile alichokitamani kuendelea kukifanya klabuni hapo kwamba alipenda apewe muda zaidi kuendelea kusalia hapo na aweze kucheza mechi nyingine zaidi akiwa kama mchezaji hapo kabla hajatimka hapo.
Msimu wake wa mwisho klabuni hapo ulikuwa ni msimu wa 10 kuwachezea matajiri hao wa Ujerumani, japo hawakuwa na msimu mzuri sana baada ya kumkubwa na majeraha mengi yaliyomfanya hadi sasa awe amecheza yapata mechi 15 tu za mashindano yote kwenye msimu huu jambo ambalo bado anajiona ana deni klabuni hapo.
Majeraha hayo ya kifundo cha mguu yalimuweka baada ya kuwafunga Benfica kwenye michuano ya klabu bingwa na tangia hapo hajapata nafasi kurejea uwanjani aweze kuonesha makali yake. Ni suala la umri pekee linamzuia ila isingekuwa hilo kwa hakika angeweza kuendelea kusalia zaidi hapo.
Kwa mapenzi aliyonayo mbele ya klabu hiyo akatamka wazi kwamba hatamani kuvaa uzi mwingine zaidi ya ule wa klabu hiyo, akimaanisha anaendelea kutamani kuvaa jezi hizo za klabu hiyo kwa wakati wote; na hiyo haijalishi itakuwa hadi lini na kwake hajali jingine zaidi ya hilo maana bado alikuwa anayapenda maisha ya hapo.
Kitu gani hatosahau?
Katika maisha yake ya soka klabuni hapo amekutana na watani wao wa ligi, Borussia mara 20 kwenye maisha yake akiwa hapo Munich. Na kitu hawezi kusahau kwenye hatua hizo ni msimu wa 2011/12 alipokosa goli dakika ya 86 ya mchezo walipokuwa nyuma kwa goli moja na goli lake likiwa kama kitu kilichokuwa kinahitajika ili waweze kuchukua ubingwa.
Hadi wakati anaachana nao alikuwa amekwishawachezea Bayern jumla ya mechi zaidi ya 300 kukiwa na mechi 700 katika soka linalotambulika pamoja na ngazi ya timu ya taifa. Kwa haya yaliyofanywa na Robben ni dhahiri kwamba anapenda soka na anatambua mchango wa klabu hiyo kwake.


Issa
Roben winga teleza