Wakati Umewadia…

Wahenga husema wakati ni ukuta ukipingana nao utaumia bure. Ule wakati wa kushuhudia michuano ya mpira wa wavu inayojulikana kama International Volleyball Federation inayoangaliwa kuanza kuchana nyavu hapo kesho huku timu zikioneshana ubabe wao kwa kiwango kikubwa cha kipekee.

Ndani ya michuano hiyo timu bora, wachezaji wenye sifa za kila aina watakuwa wakipigania taji hilo huku kila mmoja akionekana na uhitaji wa kunyanyua kombe hilo kubwa kihistoria ndani ya mchezo huo. Ni wakati ambao kila mmoja hapaswi kuukosa kutokana na historia inayojengwa.

Katika hatua hiyo itaanza michuano ya wanawake kwanza huku ikisubiriwa ya wanaume itakayokuwa kwenye ramani yake mwezi Mei mwishoni. Ni hatua muhimu sana kwa wahusika kudhihirisha ubora wao na kufuta makosa ambayo yaliwafanya kupotea kabisa msimu uliopita.

Washindi wa kombe hilo, Marekani watakuwa na kibarua kigumu hapo kesho mbele ya Wabelgiji ambao ni wazuri sana katika mchezo huo na unatazamiwa kuwa mchezo mgumu sana baina yao kutokana na historia ya kila mmoja na ubora wa wachezaji walionao ambao wana uzoefu mkubwa sana na wanaweza kubadili matokeo wakati wowote japo Marekani wanaonekana kuwa vizuri zaidi ya Ubelgiji.

Katika mchezo mwingine wa siku hiyo ya ufunguzi, China watawafuata Brazil katika mchezo unaotazamiwa kuwa mzito na wa pekee kati yao. Brazil atakuwa akitazamwa kama mwenyeji ambaye anategemewa kulipa kisasi mbele ya China ambao walimfunga 2016 kwenye michuano ya Olimpiki na kufanikiwa kuchukua medali iliyowapa heshima.

Uholanzi walipoteza mechi zao 3 msimu wa 2018 kwenye mashindano ya kidunia yanayofahamika kama World Championship lakini msimu huu pia amerejea uwanjani na atakuwa na kibarua kizito mbele ya Serbia ambao wamerudi pia vizuri ndani ya michuano hiyo. Wamejipanga vilivyo kuondoa uteja wao ndani ya michuano hiyo.

Mbali na michezo hiyo pia kutakuwa na wengine uwanjani wakitoana jasho kama Korea Kusini watakuwa wakifanya yao na Uturuki, Thailand na Ujerumani, Bulgaria na Japan, Jamhuri ya Domenika dhidi ya Warusi huku mechi nyingine yenye ushindani ikiwa ni kati ya Poland na Italy ambao wanajuana vizuri hata kwa takwimu.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.