Wayne Rooney anaendelea na maisha ya soka ndani ya klabu ya Derby County akiwa kama kocha mchezaji kwa sasa.

Baada ya Derby kumfukuza kazi aliyekuwa kocha wao Philip Cocu, Wayne Rooney alikabidhiwa jukumu la kuongoza timu hiyo kwa muda, hii ikiwa ni kipindi cha mpito kwenye timu hiyo ambayo inategemea kubadilisha umiliki kwa siku za karibuni.

Kibarua cha kwanza kwa Rooney kilikuwa dhidi ya Coventry ambapo mchezo huu ulimalizika kwa matokeo ya sare ya 1-1. Akizungumza baada ya mchezo huo, Rooney amesema ” Kwakweli sijui kama nitaendelea kuwa kocha. Kama nilivyokwisha kusema, ninajiamini katika kazi hii na ningependa kuifanya kazi hii. Isipotokea, nitabaki kama mchezaji.

Wayne Rooney, Wayne Rooney Anasubiri Uamuzi Juu Yake., Meridianbet
Rooney Akiitumikia Derby County kama nahodha wa kikosi hicho.

“Tayari tunamipango yetu na kama isipotokea (nimekuwa kocha wa Derby) basi wachezaji watakuwa wametulia wakijua mipango ya kuifanyia kazi kwa wiki chache zijazo, tutakuwa na kazi ya kufanya.

“Ninadhani muda mfupi baada ya umiliki mpya kukamilika, uamuzi utafanyika kwa sababu ninadhani unapaswa kufanyika mapema.

“Nimeelekezwa kuiongoza timu mpaka uamuzi utakapofanyika, hicho ndicho ninachokifanya. Punde uamuzi utakapokamilika sio kwa wachezaji tuu bali hata kwa wafanyakazi wengine, utakuwa ni wakati mzuri wa kujijenga na kuweka mipango vizuri kwa ajili ya baadaye.”


FURAHIA MUZIKI MTANDAONI HUKU UKITENGEZA MKWANJA!!

Mchezo wa Astro Legend unakupatia burudani ya muziki kupitia kasino ya mtandaoni ya Meridianbet. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!

Wayne Rooney, Wayne Rooney Anasubiri Uamuzi Juu Yake., Meridianbet

INGIA MCHEZONI

19 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa