Rais wa Liberia mwanasoka wa zamani wa kimataifa George Weah amempongeza mtoto wake wa kiume, Timothy Weah, baada ya klabu yake ya Lille kushinda taji la Ligi Kuu ya Ufaransa.

 

“Mimi mwenyewe kama mshindi wa taji la Ligue 1, nafahamu fika kwamba unahitaji kujitolea na kufanya kazi kwa bidii kila wiki ili kupata ushindi ,” Rais Wear alisema katika ujumbe uliowekwa katika tovuti yake rasmi ya urais.

 

“Licha ya kuumia mara kadhaa na kucheza mechi 28 , hiki ni kitu ambacho kimekuwa ndoto ya Tim.

“Tunashukuru kwamba akiwa mshambulizi wa kikosi chake , alichangia kwa kiwango kikubwa ufanisi wa Lille kuwa mabigwa kwa mara nyingine,” Bw. Weah aliongeza.

Rais Weah alichezea klabu kadhaa za Ulaya, Ikiwemo Paris Saint Germain, Monaco, AC Milan, Chelsea na Manchester City kabla ya kustaa mwaka 2004 kwenda kujitosa katika siasa za kitaifa.

Mwaka 1995 alitunukiwa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa Fifa na hatimaye kuchaguliwa kuwa rais wa nchi yake mwaka 2017.


BONASI YA 50% KILA SIKU KATIKA KASINO ZA EVOPLAY HAPA MERIDIANBET.

Meridianbet na Evoplay Kasino wanakupa bonasi ya 50% ya kiasi utakachoweka katika akaunti yako leo. Unasubiri nini ni wakati wa kupiga pesa sasa na Mabingwa.

tuchel, Tuchel :Tuna Bahati Tottenham Wametusaidia Kazi., Meridianbet

SOMA ZAIDI

3 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa