Shirikisho la soka barani ulaya, UEFA, limeamua kuandaa mashtaka rasmi ya kinidhamu kwa timu tatu za ulaya kuhusiana na sakata la European Super League.
Siku ya jana UEFA iliamua kufungua taratibu rasmi za kinidhamu kwa timu tatu za ligi ya ulaya ambazo zilishiriki kwenye ule mradi uliotikisa wadau wa soka wa European Super League. Timu tatu zilizofunguliwa mashtaka ni Barcelona, Juventus na Real Madrid.
Katikati ya mwezi April UEFA na FIFA zilipewa changamoto na kile kilichosemekana kuleta mabadiliko makubwa kwenye soka duniani. Ila mashabiki na wadau mbalimbali wa soka walipinga vikali na mwisho wa siku project hiyo ikaanguka vibaya kabisa.
Yaliyosemwa,
“Kufuatia uchunguzi uliofanywa na wachunguzi wa nidhamu na kuhusiana na kile kinachoitwa “mradi wa European Super League”, hatua rasmi za kinadhamu zimefunguliwa dhidi ya Real Madrid, Barcelona na Juventus kwa kosa kubwa la kuvunja sheria na taratibu za kisheria za shrikisho hili kubwa ulaya“, ilisema uongozi wa UEFA hapo jana.
Kulikuwa na timu 12 ambazo zilitaka kushiriki suala hili lakini tisa kati ya hizi zilijisalimisha na kujitoa moja kwa moja, huku zikiacha changamoto na migogoro mikubwa kati ya mashabiki na viongozi, lakini timu hizo tatu hazikutoa taarifa rasmi za kujitoa na hivyo shirikisho hili kubwa la soka ulaya imeamua kuandaa mashtaka dhidi yao.
Moja ya sheria zilizovunjwa zinaweza sababisha timu hizi kubwa kuondolewa kwenye mashindano rasmi ya UEFA.
BONASI YA 50% KILA SIKU KATIKA KASINO ZA EVOPLAY HAPA MERIDIANBET.
Meridianbet na Evoplay Kasino wanakupa bonasi ya 50% ya kiasi utakachoweka katika akaunti yako leo. Unasubiri nini ni wakati wa kupiga pesa sasa na Mabingwa.
Asante kwa taarifa