Timu ya Wolves imetoa taarifa kwa kocha wao mpya Bruno Lage kuwa watauza wachezaji wao wawili ili kupata pesa zaidi ya kusaidia kuongeza usajili wa wachezaji wenye damu changa klabuni hapo.
Uongozi wa Wolves umedai kuwa utawaweka sokoni na kuwauza wachezaji wao Adama Traore na Ruben Neves ili waweze kuongeza pesa kwa ajili ya usajili wa wachezaji kuelekea msimu ujao ambapo wanatamani kushika nafasi za juu zaidi.
Wolves walimaliza nafasi ya 13 katika msimu ulioisha wa 2020/2021, kinyume na namna ambavyo wamekuwa wakimaliza nafasi ya 7 kwa misimu kadhaa nyuma. Kuondoka kwa kocha wao Nuno na ujio wa Lage unamaanisha damu mpya inahitajika.
Kwa wachezaji wanaotakiwa kuuzwa, Adama Traore na Ruben Neves, Adama ambaye alijiunga na Wolverhampton Wanderers kutokea Middlesbrough anaamini kuwa msimu huu ni sahihi kwake kuondoka klabuni hapo na kutafuta changamoto mpya kwingineko.
Timu za Liverpool na Leeds United zilionekana kuhitaji huduma ya muhispania huyo, lakini kwa sasa timu ya Leeds inaonekana ipo kwenye uhitaji wa huduma hiyo. Kwahiyo bado haijajulikana sana ataangukia wapi pindi atakaposepa Wolves.
Kwa upande wa Neves, klabu kadhaa zinaonekana kuhitaji huduma yake hasa United ambao wanahitaji kujiboresha kwenye eneo lao la kati atakayesaidiana na Bruno Fernandes, kutokana na ukweli kuwa maisha ya baadae ya Pogba klabuni hapo haipowazi.
Chukua namba yako ya akaunti na kiasi cha pesa unachotaka kuweka, sogea kwenye duka lolote la Meridianbet lililo karibu nawe utasaidiwa kuweka pesa.



magdalena
Wolves wanayumba sana
Sarah
Asante kwa taarifa
Issa
Dah itapwaya