Hatimaye Xavi Hernandez anatimiza ndoto yake ya kukinoa kikosi cha FC Barcelona. Ndoto ya mkongwe huyu wa Catalunya, inakwenda kuwa uhalisia.

Barca walichukua uamuzi wa kusitisha mkataba na aliyekuwa kocha wao, Ronald Koeman baada ya kuwa na mtokeo mabaya ndani na nje ya LaLiga msimu huu. Pengine ilikuwa ni mapema kuchukua uamuzi huo lakini, nyota njema huonekana asubuhi.

Xavi Hernandez, Xavi Hernandez Kurudi FC Barcelona., Meridianbet
Xavi alipokuwa akiitumikia Barcelona kama mchezaji.

Toka kuachishwa kazi kwa Koeman, Barca walielekeza nguvu zao zote kwa Xavi Hernandez kama mtu pekee anayeweza kukiongoza kikosi cha timu hiyo. Haikuwa rahisi kumtoa Hernandez Al- Sadd kule nchini Qatar.

Baada ya maongezi na taratibu kadhaa kufuatwa, hatimaye Hernandez anarejea Camp Nou kama kocha mkuu wa timu aliyoitumikia katika maisha yake yote ya soka alipokuwa mchezaji.

Taarifa rasmi kutoka Al-Sadd imeripoti:

Uongozi wa Al-Sadd umekubali kuondoka kwa Xavi kwenda Barcelona baada ya malipo ya kimkataba kukamilika. Tumekubaliana kuwa na mashirikiano na Barcelona kwa siku za mbeleni.


MKWANJA WA KUSHATO NA AURORA BEAST HUNTER!

Mkwanja umetema ndani ya kasino za meridianbettz, Mchezo maridhawa wa Aurora Beast Hunter unakupa nafasi sawa ya ushindi leo hii, kila mzunguko una nafasi ya kuibuka mshindi, na mkwanja wako unaupata kila mzunguko utakapo kamilika.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa