Louis Saha amesifu ubora wa mchezaji mwenzake wa zamani Christiano Ronaldo na kusisitiza kwamba kocha Ole Gunnar Solskjaer anabahati kupata huduma ya mchezaji huyo aliyerejea Old Trafford.

Straika huyo wa zamani wa Mashetani Wekundu ambaye alianza kucheza United 2004 mpaka 2008, anaamini kwamba kama hupambani uwanjani basi huwezi kuwa rafiki wa Ronaldo.
“Solskjaer anapaswa kuwa na furaha Ronaldo kurejea Manchester sababu ni alien,” Saha alisema wakati wa Sport Intergrity Global Alliance (SIGA)
“Anaweza kucheza kwenye ligi yoyote na timu yoyote ulimwenguni na wakati wote atakuwa akifunga mabao, amejitolea na kujidhatiti kuliko mtu yoyote.
“Nilikuwa na uhusiano naye sababu wote tulikuwa wapambanaji, kama humpendi Ronaldo ni kwa sababu tu wewe siyo mpambanaji.
Saha pia alisema kwamba Kareem Benzema anaweza kushinda tuzo ya Ballon d’Or mwaka huu licha ya kumuona Mohamed Salah anaweza kuondoka na tuzo hiyo.
Mkwanja umetema ndani ya kasino za meridianbettz, Mchezo maridhawa wa Aurora Beast Hunter unakupa nafasi sawa ya ushindi leo hii, kila mzunguko una nafasi ya kuibuka mshindi, na mkwanja wako unaupata kila mzunguko utakapo kamilika.


