Yaliyojiri Europa…

KWENYE michuano ya ligi ndogo ya mabingwa [UEFA Europa] kila timu ilikuwa ikiwinda bafasi ya pekee sana ili kuweza kupata alama ambazo zitaisaidia kuweza kukua na kufanya vizuri kwenye michezo yao hatimaye kuibuka na ushindi katika kuwa nafasi za juu za ligi hiyo.

Katika kombe hilo ambalo lipo katika mikono ya Chelsea ambaye alinyakua ubingwa msimu uliopita, haonekani kabisa kwamba atatetea taji hilo. Kwa kawaida mechi huwa mtindo wa makundi yenye klabu nne kila moja.

Klabu ambazo zipo ndani ya michuano hiyo kutoka Uingereza ni Arsenal, Watford na Manchester United ambao watajitahidi kwa kila namna kuhakikisha hadhi ya taifa lao inatetewa kwa kasi kubwa na ya aina yake. Kwa namna ligi hiyo ilivyo kwa baadhi ya klabu huibuka na ushindi mkubwa ambao ni nafasi ya pekee sana ili kusonga mbele japo Watford walibanwa zaidi.

Arsenal walikuwa na kibarua kizito cha kuhakikisha wanachukua alama mbele ya Frankfurt ambao walifika nafasi ya fainali msimu uliopita jambo ambalo wameweza kufanikiwa kwa alama zote na wakaweza kuchukua ushindi mnono. Watford alikuwa na changamoto mbele ya Braga ambapo alishindwa kuwafunga huku United akichukua alama mbele ya Astana.

Kuna uwezekano wa klabu za Uingereza kukaa imara kwa namna ambavyo wamekuwa wakibadilika hata kihistoria kwa kufanya mambo makubwa ambayo yataendelea kubaki sehemu ya historia ndani ya taifa hilo la Uingereza ambako kwa misimu ya hivi karibuni wanaonekana kuwa katika soka lenye thamani sana.

Matokeo ya mechi zilizochezwa jana yalikuwa na magoli mengi na ya aina yake; katika kila kundi matokeo yalikuwa kama ifuatavyo: kundi A lilikuwa na matokeo ya Qarabag 0-3 Sevilla na APOEL Nicosia 3-4 F91 Dudelange, kundi B lilikuwa na matokeo ya Copenhagen 1-0 FC Lugano na Dynamo Kyiv 1-0 Malmoe FF.

Kundi C kuna matokeo ya Getafe 1-0 Trabzonspor na Basel 5-0 Krasnodar; kundi D likiwa na matokeo ya PSV Eindhoven 3-2 Sporting CP na LASK 1-0 Rosenborg; kundi E likiwa na timu za Cluj 2-1 Lazio na Rennes 1-1 Celtic; na kundi F likiwa na matokeo ya Eintracht Frankfurt 0-3 Arsenal na Standard Liege 2-0 Vitoria.

Kundi G lina matokeo ya Porto 2-1 Young Boys na Rangers 1-0 Feyenoord; kundi H lina Espanyol 1-1 Ferencvaros na Ludogorets 5- 1 CSKA Moscow, kundi I lina Gent 3-2 Saint Etienne na Wolfsburg 3-1 FC Olexandria; na kundi J lina Roma 4-0 Istanbul Basaksehir na Borussia Monchengladbach 0-4 Wolfsberger AC; kundi K lina Wolves 0-1 Braga ma Slovan Bratislava 4-2 Besiktas mwisho kabisa ni Manchester United 1-0 Astana na Partizan Belgrade 2-2 AZ Alkmaar.

Makala ijayo

Acha ujumbe