Zaidi ya Kushangilia, Shabiki Wanaojitolea kwa Jamii

Kama umewahi kusikia kuwa soka ni zaidi ya kuwepo dimbani na kushangilia, basi ipate hii leo! Soka lina mambo mengi sana ambayo huendelea na ndani ya uwanja na nje ya viwanja. Watu huwapata marafiki wapya na kudumu nao kupitia soka, watu hurejesha furaha zao wanazo poteza kwa mda mrefu. Soka ni mapenzi! Umeshawaji kujivunia kuwa shabiki wa timu yako? kama ndiyo ni kwa lipi?

Wakati ukijifikiria maswali hayo hapo juu na kujitahmini kama mwanamichezo au mwanasoka na shabiki wa timu fulani, hapa nakuhabarisha mfano wa mashabiki wapenzi wa Manchester City ambao wameamua kuunganishwa na ushabiki wao kuisaidia jamii.

Jamii imekuwa ikihitaji msaada katika changamoto mbali mbali. Katika kipindi hiki ambacho dunia inapambana na virusi vya Corona, baadhi ya nchi zimeamua kuzuaia Raia wake kutoka nje na kusalia majumbani kwao ili kupumbuka kasi ya maambukizi.

Mahabiki wa Man City wamekuwa wakitoa msaada wa chakula kwa watu wenye uhitaji kipindi hiki wakiwa ndani. Mashabiki hawa wamekuwa wakifanya kazi hii ya kujitolea kusaidia umma siyo tu kipindi hiki, bali ni kwa mda sasa, na kwa takribani miezi sita iliyopita wameweza kutoa mafungu 42000 ya vyakula kwa akli ya kuwasaidia watoto wenye uhitaji kwa mji wa Manchester pekee.

Mashabiki wa Vilabu vingine wamevutiwa na kuona namna wanavyoweza kufanya jitihada za pamoja kuwafikia watu wengi zaidi wenye uhitaji. Huu ni mfano mzuri wa ushabiki ni zaidi ya uwanjani na soka ni zaidi ya vyenga, magoli au mataji, ni upendo na nyenzo ya kurudisha matumaini na kuwaunganisha watu.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.