Macho ya Inter na Roma Yatua kwa Thomas Partey

Klabu za Inter na Roma zinaungana na Manchester United na Arsenal wanaotajwa kuwa wanavutiwa na kiungo wa Atletico Madrid Thomas Partey.

Kwa mujibu wa chapisho la Mundo Deportivo, raia huyu wa ghana amezivutia klabu kadhaa za Italia na Uingereza.

Nyota huyu ana mkataba na klabu ya Atletico hadi Juni mwaka 2023. Mkataba wake unatajwa kuwa na dau la kumnunua la Euro milioni 50 lakini mazungumzo zaidi yanaweza kukamilisha biashara yake.

Kiungo huyu alitokea kwenye klabu ya vijana ya Atletico Madrud na mpaka sasa amecheza mechi 35 msimu huu, na kuchangia magoli 3 na asisti 1.

Mundo Deportivo wanasisitiza kuwa Inter Milan walihitaji kumsajili nyota huyu mapema zaidi na walishafanya majaribio kadhaa kukamilisha uhamisho wake, huku vilabu vya Manchester United, Roma na Arsenoal wakiunga tela hivi karibuni kuonesha kuvutiwa naye.

3 Komentara

    Asante meridianbet

    Jibu

    Thomas yuko vizuri

    Jibu

    Thomas partey ni mchezaj mzr tuu

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.