Wajumbe sita wa bodi ya Barcelona wamejiuzulun akumwambia Raisi Josep Maria Bartomeu hawana furaha kwa nmna klabu inavyoendeshwa.
Kwenye barua ya pamoja, wajumbe wote sita wameongelea kuhusu kuporomoka kwa hali ya uchumi katika kipindi hiki cha Corona kama janga la klabu.
Wamepinga namna skendo ya ilivyochukuliwa mwezi Februari, wakati klabu ilipolazishwa kukataa kuwa wameajiri kampuni kwaajili ya kushambulia wachezaje wake kwenye mitandao ya kijamii, na wameitaka Barca kuitisha uchaguzi, kwaajili ya Raisi mpya.
Emili Rousaud na Enrique Tombas – ni wawili kati ya makamu wa raisi wanne wamejiuzulu na wakurugenzi wanne, Silvio Elias, Josep Pont, Jordi Calsamiglia na Maria Teixidor.
“Tumefikia hatua hatukubali namna klabu inavyoendeshwa katika kupambana na changamoto muhimu za sasa na hapo baadae, hasa kipindi hiki cha mlipuko,” barua yao imeleeza.
“Lakini pia tunasikitishwa na tukio la akaunti ya mitandao ya kijamii inayojulikana kama ‘Barcagate’.”
“Huu ni wakati wetu wa mwisho wakutumikia klabu, tunashauri uitishwe uchaguzi wa haraka, ili klabu ipate Raisi mpya ambaye ataweza kuiendesha namna nzuri na kuweza kutatua changamoto za hapo baadae.”
isha
Duuh balaa limeanza