Imechukuia zaidi ya miezi miwili kwa mshambulaiji wa Juventus Cristiano Ronaldo kumaliza kugawa zawadi ya kompyuta aina ya Imac kwa kikosi kizima cha Juve, hii ni baada kupata adhabu hiyo katika mchezo ligi ya klabu bingwa Ulaya (UEFA Champions League) msimu wa 2018 waliyo cheza wao dhidi ya klabu ya Valencia inayoshiriki ligi kuu nchini Hispania.
Ronaldo alifanya hivyo kufuatia sheria iliyowekwa na aliyekua kocha mkuu wa kipindi hicho Massimiliano Allegri iliyomtaka kila mchezaji kugawa zawadi kwa wachezaji wenzake kila anapopata kadi nyekundu.
Golikipa wa Juventus Wojciech Szczesny akiongea na Polish Television alisema “Ndio, wote tunazo. Imechukua muda mrefu kidogo kwasababu Ronaldo aliamini hakufanya kosa ambalo lingepelekea kosa lake kupata kadi nyekundu”
Golikipa huyo wa zamani wa timu ya Chelsea inayoshiriki ligi kuu nchini Uingeleza alishawahi pia kukutwa na rungu kama hilo baada ya kutiliza siku moja baada ya ile iliyopangwa kufika kambini. “nakumbuka ilikua Jumanne, ila mimi nilifika kambini Jumatano ambapo licha ya kuchelewa siku moja bado nilichelewa tena lisaa limoja na nusu.”

Aliendelea kwa kusema “Allegri aliniita na kusema kua kila mtu alikua ananisubiri, nimechelewa kwa zaidi ya lisaa limoja na nusu hivyo natakiwa kumnunulia kila mchezaji hedi foni za BEATS“
Kwa sasa Juventus inaongozwa na aliyrkua kocha mkuu wa zamani wa Chelsea Maurizio Sarri , ambapo Sarry na wachezaji wa Juventus wamekubaliana kukatwa mishahara yao kunusuru hali ya kiuchumi ya timu yao Juventus.


David pere
Hii kweli hatari tupu Yani Kuna zawadi moja kwenye kadi nyekundu duh