Messi ni Nyota wa Kizazi Hiki

Huku mabishano yakiwa bado yanaendelea duniani juu ya yupi bora kati ya Messi na Ronaldo kuna wengine wanaendelea kulishikia nyundo jambo hilo kwa kuona kwamba hakuna haja ya kuendelea kuwazungumzia wawili hao kwa sabahu kila mtu ana heshima na misingi yake kutokana na kile alichoweza kukifanya katika soka.

Lakini wapo wengine wanaoona mmoja yupo juu ya mwingine japo vigezo vinavyowekwa ni vilevile ambavyo mwingine anavyo tayari na huenda tayari amekwisha vivuka kwa asilimia kubwa sana. Hilo ni jambo ambalo wengi wanalizungumzia bila kuangalia nyuma ya pazia kuna vitu gani.

Si suala la kubisha kwamba kwa wakati uliopo ambao Ronaldo umri umeweza kusogea kwa kiasi fulani, Messi anaonekana akivunja rekodi ambazo tayari Ronaldo alikuwa amekwisha zifikia kwa wakati wake, ambao haukuweza kuzungumzika kabisa kwamba anachofanya ni bora zaidi ya mwingine.

Gundogan ni kati ya wachezaji ambao wanaamini kwamba Messi ni mchezaji kutoka sayari nyingine lakini kwa upande mwingine huwezi kuzungumza suala hilo mbele ya wachezaji wa Real Madrid ambao wanaujua fika mchango wa Ronaldo kwenye timu hiyo ambao hadi leo bado kuna nafasi yake inaonekana.

Upande wa tuzo wawili hao wameweza kulingana huku Messi akiwa na Ballon d’Or tano na hata mpinzani wake wa karibu akiwa ameweza kufikia kiwango kama hicho. Kwa sasa ni wakati wa Messi kuwika kwa kiasi fulani kwa sabahu Ronaldo hatupo ndani ya ligi hiyo na zaidi umri wa nyota huyo umesogea kwa namna fulani.

Kinachomfanya Gundogan kuamini kwamba Messi ni nyota namba moja kwake katika soka duniani ni kupitia ule uwezo binafsi ambao ndio unaitwa kipaji cha mpira, huku ikiwa ni tofauti kidogo na Ronaldo ambaye jitihada na kujituma kumeweza kumpa mafanikio ya pekee sana katika soka lake.

Kwa uhalisia uliopo hawa wawili ni alama kubwa sana ya soka na kila mmoja anatakiwa kupewa heshima yake kubwa na ya pekee sana kwa sababu aliyoyafanya ni makubwa sana na yanafaa kuweza kuheshimiwa na kila mmoja. Sio rahisi kuzivunja rekodi za wawili hao kwa siku za usoni kwa kizazi hiki ambacho kinachipukia kwa sasa itachukua wakati mrefu kuweza kufikia na kuwa na watu kama hawa japo lazima itaweza kutokea.

3 Komentara

    Messi mkali sana

    Jibu

    Wote ni bora pia kiwango nikimoja ikiwa wao wanaona kila mmoja amemzidi mwezake

    Jibu

    Asante kwa taarifa

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.