Manchester United wameripotiwa kumweka katika malengo yao nyota wa Dortmund Jardon Sancho na wana matumaini kuwa watamsajili staa huyu. kama United wataamua kumsajili basi inawezekana wakalazimika kumnunua kwa dau la kuvunja rekodi yao ya manunuzi kufuatia onyo alilotoa mkurugenzi wa klabu ya Borrusia Dortmund.

Boss huyu wa dortmund Joachim Watzke ameweka wazi kuwa hawatakuwa wakikaribisha klabu yeyote kwenye makubaliano ya kumnunua staa huyu. Dortmund ambayo ilimnunua staa huyu mwenye miaka 20 kwa Euro milioni 8 miaka mitatu iliyopita haipo tayari kumuuza, na wanampango wa kuendeelea kumtumia na japokuwa wapo tayari kumpatia kile anachohitaji.

Wakati klabu ya Man United ikimhitaji Sancho kwa ajili ya kuboresha kikosi chake, staa huyu pia alibainisha nia yake ya kutaka kuondoka klabuni hapo.

Mkurugenzi huyu anasema kuwa wao walikwishaweka wazi tangia mapema, kabla ya Janga hili la virusi vya Corona kuwa staa huyu atabaki klabuni hapo. Aliweka msisitizo kuwa hata klabu ikiwa tajiri namna gani na hali halisi ya uchumi ilivyoathirika hawaamini kama kuna klabu itasogea kukaa meza moja kumnasa kinda huyo.

Sancho kwa sasa anatajwa kuwa na thamani ya Euro milioni 100 katika soko, wakati klabu hiyo ikitarajiwa kuwa itapandisha hadi Euro milioni 120. Hii itakuwa ni zadi ya ada ya Paul Pogba kama Man United wakiamua kumchukua. Laikini bosi huyu wa Dortmund anasema hawatamuuza yeyote chini ya kiwango.

Man United walikuwa wanatarajiwa wengeenda kwenye meza ya mazungumzo ili kuona namna wanavyoweza kukubaliana kuhusu mchezaji huyo. Ujumbe huu unaweza kubadilisha mipango ya United wakaamua kufunika kombe mwanaharamu apite.

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa