Ziyech Atangaza Kustaafu Timu ya Taifa.

 

Mshambuliaji wa Morocco Hakim Ziyech amethibitisha atajitolea nguvu zake kwaajili ya klabu yake ya Chelsea, na hataichezea nchi yake tena.

 

Ziyech, 28 aliondolewa kwenye kikosi cha Morocco kilichoshiriki Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON hivi karibuni na kocha Vahid Halilhodzic, ambaye alimtuhumu mchezaji huyo kwa utovu wa nidhamu.

Morocco itamenyana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo mwezi Machi kwa mechi ya mchujo wa nyumbani na ugenini kuwania nafasi moja kati ya tano ambazo mataifa ya Afrika yanawania katika Kombe la Dunia la 2022 nchini Qatar.

Ziyech yuko Umoja wa Falme za Kiarabu na Chelsea kwa ajili ya kampeni ya Kombe la Dunia la Vilabu na alitoa kauli yake katika mahojiano na shirika la utangazaji la Abu Dhabi Sports.

“Sitarudi kuitumikia timu ya Taifa,” alisema Ziyech.

 

“Uamuzi wangu ni wazi na wa mwisho, nitakuwa nikizingatia klabu yangu,” aliongeza.

Kocha wa Morocco, Halilhodzic alieleza chaguo lake baada ya kuondolewa kwa timu yake katika robo fainali ya AFCON.

 

“Siwezi kumwita mchezaji ambaye anaweza kuharibu kundi, hata kama angekuwa Lionel Messi,” alisema.

Alisema pia kwamba Ufaransa ilishinda Kombe la Dunia mnamo 1998 na 2018 baada ya kuwaweka kando wachezaji wao bora.

“Mimi sio kocha wa kwanza kuamua hii,” aliongeza.


KASINO YA MTANDAONI: EMOTICOINS SABABU YA KUVUNA ZAIDI.

Haijawahi kuwa rahisi hivi kwenye safari yako ya kuvuna mkwanja, kasino maridhawa ya meridianbettz inakuletea mchezo wa Emoticoins unaokupa nafasi ya kufanya safari yako kuwa rahisi zaidi. Wakati ni wako nafasi ni yako na Emoticoins.

senegal, Senegal Mabingwa AFCON 2021., Meridianbet

CHEZA HAPA.

Acha ujumbe