Shilikisho la mpira wa miguu barani ulaya UEFA wanatarajia kuhamisha mchezo wa fainali uliopangwa kuchezwa nchini Russia jijini St Petersburg kutokana na tuhuma za uvamizi.

UEFA imearisha maonyesho yao yaliopangwa kufanyika katika jiji la St Petersburg tarehe 28 may, shirikisho hili limeongeza msukumo wa kutafuta jiji jipya ambalo litaendesha fainali ya mashindano hayo, baada ya Russia kuvuka mpaka na kuingi nchini Ukraine.

UEFA

Video ambazo zimerokodiwa usiku wa jana na kuachiwa leo siku ya jumanne zikionyesha magari ya kivita ya kutoka nchini Russia na kuvuka mpaka wa Ukraine, kwenye ukanda ambao unamilikiwa na waasi kwa ajiri ya mazoezi ya amani, imefanya UEFA kukaa kikao cha kutafuta hitimisho ikiwa waendelee na Russia au wahamishe fainali hizo.

Jiji la London kupitia uwanja wake wa Wembley ndio linapigiwa chapuo kuchukua nafasi ya kuandaa fainali ya ligi ya mabingwa, pia kuwa uwezekano wa fainali hiyo kuchezwa jijini Istanbul kutokana na fainali ya mwaka jana kuhamishwa kutokana na mlipuko wa Uviko-19.

UEFA

Pia kuna mazungumzo ya kati Dynamo Kiev na Sporting Lisbon kuhusu mchezo wa vijana wa hatua 16 bora ambao ulipangwa kufanyika nchini ukraine march 2, ikwa utaendelea kama ulivyopangwa au kuhamisha.

Zenit St Petersburg ndio klabu pekee kutoka ukanda wa Russia kubaki kwenye mashindano yanayoandaliwa na UEFA, pia mpaka sasa kwenye mchezo wa kwanza wamefungwa kwa 3-2 dhidi ya  Real Betis.


SHINDA IPHONE 12 NA KASINO YA AVIATOR

Meridianbettz na Aviator wanakupa mchongo wa kuibuka na iPhone 12 katika kasino ya Aviator itakayodumu kwa siku 7. Kuwa rubani wa Aviator na ujishindie!

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa