Argentina Bingwa Kombe la Dunia 2022

Timu ya taifa ya Argentina imefanikiwa kubeba taji la michuano ya kombe la dunia iliyofanyika nchini Qatar mwaka 2022 baada ya timu hiyo kuifunga timu ya taifa ya Ufaransa kwa mikwaju ya penati.

Mchezo wa fainali uliopigwa katika dimba la Lusail ulikua mchezo mkali na ambao umevutia watu wengi sana baada ya kushuhudia matukio mazuri zaidi katika mchezo huo wa fainali, Mchezo huo ulivutia watu zaidi pale ambapo ulionekana umemalizika lakini haukua umemalizka.

Timu ya taifa ya Argentina ilifanikiwa kupata mabao mawili ya haraka kipindi cha kwanza kupitia kwa Lionel Messi kwa mkwaju wa penati na Angel di Maria, Ambapo mpaka timu hiyo inakwenda mapumziko ilikua inaongoza kwa mabao mawili kwa bila.argentinaKipindi cha pili kiliendelea kwa timu ya taifa ya Argentina kuendelea walipoishia na kutawala mchezo kwa kiwango kikubwa, Mpaka pale dakika kumi za mwisho timu ya taifa ya Ufaransa ilipofufuka kwa kupata goli la kwanza dakika ya 80 kwa mkwaju wa penati kupitia Kylian Mbappe na kuongeza bao la pili dakika ya 81 ya mchez na matokeo kua mbilimbili.

Maajabu ndani ya dimba la Lusail yalitokea baada ya Ufaransa kutoka nyuma kwa mabao mawili kwa bila na kufanikiwa kurudisha mabao yote ndani ya dakika mbili kupitia kwa staa wao Kylian Mbappe.argentinaTimu hizo mpaka dakika tisini zinamalizika mchezo ulikua na matokeo ya kushangaza baada ya Ufaransa kurudisha mabao yote mawili na kufanya mchezo huo kwenda dakika 120 za nyongeza ambapo mpia mchezo huo ulishindwa kuamuliwa, Hiyo ni baada ya Argentina kupata bao la tatu kupitia Lionel Messi na Ufaransa kusawazisha kupitia kwa Kylian Mbappe.

Mechi iliamuliwa kwa mikwaju ya penati baada ya dakika 120 kutamatika matokeo yakiwa 3 kwa 3, Na kwenye mikwaju ya penati shujaa wa Argentina alikua yule Emiliano Martinez ambae aliokoa penati ya Kingsley Coman na Aurellien Tchouameni kukosa pia na kuifanya timu hiyo kushinda kwa penati 4-2.

Argentina wametawazwa rasmi kua mabingwa wa michuano ya kombe la dunia mwaka 2022 iliyofanyika nchini Qatar, Pia kuongeza taji la tatu la michuano hiyo baada ya kupita takribani miaka 37 ikiwa mara ya mwisho kubeba taji hilo mwaka 1986.

Acha ujumbe