Beki wa zamani wa klabu ya Bayern Munich na timu ya taifa ya Ujerumani Holger Badstuber amesema timu ya taifa ya Croatia ina uwezo wa kumsimaisha Messi pamoja na timu ya taifa ya Argrntina kwenye mchezo wa nusu fainali ya kombe la dunia leo.
Timu ya taifa ya Argentina itamenyana na timu ya taifa ya Croatia kwenye mchezo wa nusu fainali ya kombe la dunia usiku wa leo mchezo unaotarajiwa kua na ushindani mkubwa sana kutokana na ubora wa vikosi vyote viwili.Gwiji huyo wa zamani wa klabu ya Bayern Munich anaamini timu ya taifa ya Croatia ndio timu pekee kwenye michuano hii ambayo inaweza kumzuia Lionel Messi na timu ya taifa ya Argentina kwa ujumla kutokana na ubora timu hiyo ambayo imekua nayo.
Timu ya taifa ya Croatia imeonekana ni timu ambayo imejengeka sana kuanzia safu ya ulinzi, eneo la katikati ma pia safu ya ushambuliaji hivo kuonekana moja ya timu ambazo zina uwiano mzuri zaidi kwenye kila eneo uwanjani.Katika mchezo wa leo usiku wa nusu fainali utakua unawaangalia zaidi manahodha wawili kutoka Argentina Lionel Messi na Luca Modric kutoka Croatia kuona ni nani ataweza kuibeba timu yake kwenda kwenye hatua ya fainali ya michuano hiyo mwaka huu.