Zanetti: Messi Kubeba kombe la Dunia sio Sababu ya Kumshinda Maradona

Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Argentina na klabu ya Inter Milan ya nchini Italia Javier Zanetti amesema kua Lionel Messi kubeba taji la kombe la dunia sio sababu ya kumzidi gwiji Diego Maradona.

Mchezaji wa klabu ya PSG Lionel ambaye amechukua kombe la dunia juzi baada ya kuifunga timu ya taifa ya Ufaransa kwa mikwaju ya penati, Na kufikia rekodi ya gwiji Diego Armando Maradona ambaye alibeba ubingwa huo mwaka 1986 akiwa na timu hiyo.zanettiKutokana na kiwango bora alichokionesha Lionel Messi kwenye michuano ya kombe la dunia mwaka huu kitu kilichokifanya kupigilia msumari  ule mjadala wa kua mchezaji bora zaidi kutokea kwenye mpira. Lakini imekua tofauti kwa Zanetti ambaye anasema hakuna kitu kilichobadilika kwa upande wake.

Gwiji Zanetti alienda mbali na kusema kua yeye hapendi sana watu wanavyowashindanisha Maradona na Messi na zaidi yeye anaamini Waargentina wanapaswa kujivunia kua wachezaji wawili bora zaidi duniani wanatoka nchini kwao.zanettiLionel Messi baada ya kubeba kombe la dunia nchini Qatar siku ya jumapili imemfanya imeibua mijadala mingi sana baada ya wengi kuamini kua ndio mchezaji bora kuwahi kutokea, Lakini mijadala imekua mingi kwani kuna upande unaamini Messi kubeba kombe la dunia hakumfanyi kua bora zaidi ya Pele, Maradona pamoja Cristiano Ronaldo.

Acha ujumbe