Tyrell Malacia amezungumzia uhusiano wake wa karibu na mchezaji mwenzake mpya wa Manchester United Lisandro Martinez.

Wachezaji hao wawili walifika Old Trafford kutoka Eredivisie majira ya joto, na Malacia akajiunga kutoka Feyenoord huku Martinez akiungana na bosi wake wa zamani wa Ajax Erik ten Hag.

Baada ya kuanza kwa taratibu, wawili hao kwa haraka wamekuwa sehemu muhimu ya safu mpya ya ulinzi chini ya Ten Hag, huku Malacia akimuweka nje Luke Shaw katika beki wa kushoto, na Martinez kwa sasa akimuweka benchi nahodha Harry Maguire.

Akizungumza na vyombo vya habari vya klabu hiyo, Tyrell alisema anapenda kufanya kazi na Martinez.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 alisema: “Ndio, tunazungumza sana kuhusu soka na ni mtu mzuri. Ni mlinzi mzuri na anatupa nguvu. Uliona hivyo kwenye mchezo dhidi ya Liverpool pia, kwa hivyo napenda sana fanya naye kazi.”

Alipoulizwa kama Martinez ni shujaa nje ya uwanja, Tyrell anacheka: “Hapana! Yeye ni mkimya kidogo. Anatabasamu na kuongea sana (akiwa uwanjani) lakini hayuko hivyo nje ya uwanja.”

Wachezaji wote wawili watakuwa na matumaini ya kutunza nafasi zao huku wakijaribu kuiongoza United kupata ushindi wa nne mfululizo wakati Arsenal watakapowafuata Old Trafford Jumapili.

