Tanzania Yatinga Robo Fainali Yaichapa Japan 3-1 Uturuki

Timu ya taifa ya walemavu ya Tanzania imetinga robo fainali ya kombe la dunia kwa watu wenye ulemavu baada ya kuichapa Japan 3-1 katika mchezo wa hatua ya 16 bora mashindano ya kombe la Dunia yanayoendelea nchini Uturuki.

Leo Alhamisi, timu ya Taifa ya watu wenye ulemavu ‘Tembo Warriors’ itakuwa uwanjani kwenye uwanja wa TFF Riva jijini Instanbul kumenyana na Haiti ikiwa ni mchezo wa hatua ya robo fainali ya mashindano ya kombe la Dunia yanayoendelea nchini Uturuki.

Tanzania sasa itakutana na Haiti waliomfunga Marekani 6-2, katika mchezo wa robo fainali utakaopigwa kesho.
Wawakilishi hao wa Afrika walianza kwa kwenda sare ya 0-0, wakachapwa na Poland 3-0, kabla ya kuichapa Uzebkistan 2-0 na kutinga 16 bora.

Huenda ikakutana na Brazil katika nusu fainali, iwapo itaitoa Haiti. Brazil yenyewe inakutana na wawakilishi wengine wa Afrika, Angola.

Ukiacha Tanzania, Angola, wawakilishi wengine wa Afrika waliotinga nusu fainali ni Morocco iliyoitwanga 4-0 Argentina.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.