Nabi Alia na Ratiba Kuelekea Mechi ya Shirikisho

Kocha wa klabu ya Yanga Nasserdine Nabi amelalamikia ratiba ya ligi kuu Tanzania Bara kuelekea mchezo wao wa kombe la shirikisho dhidi Club Africain kutoka nchini Tunisia.

Kocha huyo wa klabu ya Yanga amelalamikia kua ratiba ya Ligi kuu nchini imekua ngumu na kusababisha kukosa muda wa kujiandaa vizuri dhidi ya Wapinzani wao hao kutoka nchini Tunisia ambapo ni nyumbani kwa kocha huyo kiasili.nabiKlabu ya Yanga imecheza michezo takribani minne ndani ya siku chache kitu ambacho mwalimu Nabi amekilalamikia,Pia  kusababisha  majeraha kwa baadhi ya wachezaji  wawili kwenye kikosi chake kutokana na kucheza michezo mingi ndani ya siku chache.

Nabi amekua kocha wa pili amekua wa klabu hiyo kulalamikia ratiba ngumu hapo mwanzo kocha msaidizi wa klabu hiyo Cedric Kaze pia alilalamikia ratiba kuwabana klabu hiyo kuelekea mchezo wao wa kimataifa. Mwalimu Kaze yeye aliamini shirikisho lilipaswa kuwasaidia Klabu hiyo na kuwapa muda wa kupumzika kwakua wanawakilisha taifa.nabiKocha huyo amezungumza na waandishi wa habari leo hii kuelekea mchezo wa dhidi ya Club Africain ambao utapigwa kesho katika dimba la Benjamin Mkapa, Amesema hawezi kutumia sababu ya ratiba lakini ukweli hawapata mda wa kujiandaa zaidi wameweza tu kumsoma mpinzani wao.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.