Simba Queens jana walipata ushindi wao wa kwanza kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, mashindano yanayoendelea nchini Morocco.
Simba walishinda mchezo huo kwa mabao 2-0. Opah Clement akiweka rekodi ya kufunga bao la kwanza kwenye mashindano hayo kwa Simba Queens.
Huku Nigerian Winga Olaiya Barakat akifunga bao la pili kwa mkwaju wa penalty baada ya Burundian Maestro Mariamu Joelle Bukuru kufayiwa madhambi na VAR kuwapa tuta Simba.
Simba sasa anatakiwa kumfunga Green Buffaloes kesho kutwa Novemba 5 ili kuweza kuungana na AS FAR RABAT ambao ndiyo vinara wa kundi wakiwa na alama 6.
Simba na Green wote wana alama 3. Utofauti ni kwamba Green ana mabao mengi ya kufunga ambayo ni Matano wakiwa wamefungwa mawili. Huku Simba wamefunga mabao mawili na kufungwa moja.

