Nahodha wa kikosi cha Tanzania Prisons, Benjamin Asukile amesema kuwa wao kama wachezaji hawatamani kuona kile kilichotokea msimu uliopita kijirudie tena.
Msimu uliopita Prisons walinusurika kushuka daraja ambapo walicheza hatua ya mtoano dhidi ya JKT Tanzania na kufanikiwa kubaki ligi kuu.

Leo kikosi cha Tanzania Prisons kinashuka kwenye dimba la Uhuru kukipiga dhidi ya Ruvu Shooting ukiwa ni mchezo wa ligi kuu.
Asukile amesema kuwa wao kama wachezaji kwa msimu huu wamejipanga kupata ushindi katika kila mchezo ili yale ya msimu uliopita yasijirudie.
“Sisi tupo salama tunamshukuru Mungu, tumekamilisha maandalizi yetu ya kujiandaa na mchezo dhidi ya Ruvu Shooting.
“Kama wachezaji kwa msimu huu tumejiwekea malengo kuwa tunahitaji kuisaidia timu kupata matokeo katika kila mchezo ili kuhakikisha yale yaliyojitokeza msimu uliopita hayajirudii tena.
“Ruvu ni timu nzuri ina wachezaji wazuri pia wapo kwenye Uwanja wao wa nyumbani lakini tutaenda kupambana kwa ajili ya kuhakikisha tunapata matokeo.”

