Yanga Yasepa Tunis

Baada ya kuweka kambi kwenye mji wa Sousse nchini Tunisia, kikosi cha Yanga leo kimeondoka kuelekea Tunis kwa ajili ya mchezo wao wa michuano ya Shirikisho barani Afrika.

Yanga kabla ya kuondoka katika mji wa Sousse walifanya mazoezi ya kujiweka fiti leo asubuhi tayari kwa ajili ya safari hiyo ya kuelekea Tunis ambapo mchezo huo utapigwa.

Kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nassredine Nabi kinatarajia kucheza mchezo huo wa marudiano Novemba 9 mwaka huu dhidi ya Club Africain ya nchini Tunisia.

Ikumbukwe kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa Novemba 2 mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkapa ulimalizika kwa suluhu ya timu hizo kutokufungana.

Yanga ili waweze kufuzu katika hatua ya makundi ya michuano ya Shirikisho barani Afrika wanapaswa kupata sare au kushinda kwenye mchezo huo wa marudiano.

Acha ujumbe