JKT Wapania Kurejea Ligi Kuu

Kocha Msaidizi wa kikosi cha JKT Tanzania, George Mketo amefunguka kuwa mipango yao ni kuhakikisha wanapata nafasi ya kurejea ligi kuu kwa msimu ujao.

JKT ambayo inashiriki ligi ya Championship inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo ikiwa imekusanya pointi 19 baada ya kucheza mechi nane.

Akizungumzia mipango yao, Mketo alisema: “Kwanza tunamshukuru Mungu kikosi kipo vizuri kinaendelea na maandalizi ya mchezo ujao ambao tutacheza siku ya ijumaa.

“Kila mchezo kwetu ni fainali hivyo tumejipanga kwa msimu huu kuhakikisha kwamba tunapata nafasi ya kushiriki ligi kuu kwa msimu ujao.

“Msimu uliopita benchi lilikuwa lingine na walijitahidi kwa nafasi yao kupata nafasi ya kushiriki ligi kuu ikashindikana lakini sisi tunahitaji kupata nafasi ya kupanda moja kwa moja hivyo ili kutimiza hilo tunapaswa kushinda kila mchezo uliopo mbele yetu.”

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.