Gwiji wa zamani wa Man United Lois Saha amesema mjadala wa Ronaldo na Messi haujaisha baada ya Messi kubeba kombe la dunia, Huku akiamini bado Ronaldo ni bora.
Louis Saha ambaye amewahi kucheza klabu ya Manchester United na staa Cristiano Ronaldo amesema anaamini kua nyota mwenzake huyo kwenye kikosi cha United ni mchezaji bora zaidi kwake zaidi ya Lionel Messi kutokana na aliyoyafanya kwenye mpira wa miguu.
Gwiji Louis Saha anasema kwake Cristiano Ronaldo ni mchezaji aliekamilika zaidi kwasababu nyota huyo anaweza kufanya vitu vingi zaidi uwanjani kwa ubora bila kuhitaji usaidizi, Lakini yeye anaamini Messi anahitaji msaada mkubwa ili kufanya vizuri.
Kumekua na mjdala mkubwa sana duniani baada ya staa Lionel Messi kubeba kombe la dunia na timu ya taifa ya Argentina, Wengi wakiamini mjadala wa nani mchezaji bora zaidi kati yake na Ronaldo umnemalizika lakini imekua tofauti kwa upande wa Louis Saha.
Gwiji huyo wa zamani wa Man United ameibua mjadala mzito kwani wadau na mashabiki wengi wa mpira wa miguu wamemshambulia kwa kudai kua amesimama upande wa Ronaldo kwakua walicheza pamoja ndani ya United na hajaongea uhalisia.

