Staa wa klabu ya Real Madrid Eden Hazard ameonekana katika mazoezi ya klabu yake ya Real Madrid mapema leo ikiashiria sasa mchezaji huyo amerejea kutoka kwenye majeraha yaliyokua yanamkabili.
Eden Hazard alitangazwa kupata majeraha mapema ndani ya mwezi huu na ikaelezwa atakua nje ya uwanja kw amuda usiojulikana, Majeraha ya mchezaji huyo yalitarajiwa kua makubwa na kumuweka nje ya uwanja kwa muda mrefu lakini ameweza kurejea ndani ya wiki mbili.
Staa huyo alipata tatizo katika goti lake la kushoto na kuelezwa atakua chini ya uangalizi wa madaktari ndani ya klabu hiyo kutokana na jeraha lake hilo alilolipata, Lakini kwenye hali isiyotarajiwa mchezaji ameweza kurejea mapema uwanjani.
Eden Hazard amekua akiandamwa na majeraha tangu ajiunge na klabu ya Real Madrid mwaka 2018 kitu kinachomfanya kushindwa kufurahia mpira wake ndani ya klabu hiyo, Mchezaji huyo amepata majeraha takribani mara 18 tangu ajiunge na wababe hao wa soka nchini Hispania.
Mchezaji Eden Hazard amekua akikosa nafasi ya kuanza ndani ya kikosi cha Real Madrid tangu kipindi cha kocha Zinedine Zidane na mpaka wakati huu wa kocha Carlo Ancelotii na hiyo imesababishwa na yeye kupata majeraha mara kwa mara ndani ya klabu hiyo.

