Ancelotti: Benzema Asingecheza Mchezo wa Liverpoo kama Ungekua Kesho

Kocha wa klabu ya Real Madrid Carlo Ancelotti amesema kua mshambuliaji wake hatari Karim Benzema asingeweza kucheza mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya klabu ya Liverpool kama mchezo huo ungechezwa kesho.

Kocha Ancelotti amemuondoa Karim Benzema kwenye kikosi kitakachomenyana na klabu ya Osasuna wikiendi hii katika mchezo wa ligi kuu ya Hispania, Hii inaonesha wazi kabisa kua mshambuliaji huyo hayuko fiti na hiyo ni baada ya kucheza mchezo wa katikati ya wiki dhidi ya klabu ya Elche.AncelottiMshambuliaji Karim Benzema amekua akiandamwa na majeraha ya mara kwa mara tangu kuanza kwa msimu huu huku akikosa michuano ya kombe la dunia yaliyofanyika nchini Qatar, Huku akikosa mchezo mmoja wa Spanish Super Cup pamoja na mchezo waliopoteza dhidi ya klabu ya Real Mallorca wiki iliyomalizika.

Kocha Carlo Ancelotti amesema kua nyota huyo angekosekana katika mchezo wa kesho dhidi ya Osasuna na hiyo ni kutokana na kutokua fiti kwa mchezaji huyo, Rasmi sasa Karim Benzema atakosekana katika mchezo wa ligi kuu dhidi ys Osasuna.AncelottiAncelotti inaonekana ameamua kuupa umuhimu mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya klabu ya Liverpool katika hatua ya 16 bora utakaopigwa katika dimba la Anfield jumanne ijayo, Kwani ameamu kumpumzisha Benzema kwa kuhofia kuumia kwa mchezaji huyo ili asije kukosekana katika mchezo dhidi ya Liverpool.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.