Rais wa klabu ya Napoli Auriello de Laurentiis amesema kocha wa klabu hiyo raia wa kimataifa wa Italia Luciano Spalletti hawezi kuondoka ndani ya timu hiyo mwishoni mwa msimu huu.
Kocha Spalletti amekua na wakati mzuri ndani ya klabu ya Napoli na kufanikiwa kutengeneza timu bora kabisa ambayo imekua tishio barani ulaya, Lakini kulianza kuzuka kwa taarifa mbalimbali kua kocha huyo anaweza kutimka ndani ya klabu hiyo kitu ambacho Laurentiis amekanusha vikali.
Kocha huyo anatajwa kuongezewa mkataba mpya ndani ya klabu hiyo wiki chache zijazo kutokana na mazungumzo kukamilika baina ya klabu hiyo na kocha huyo, Raia huyo wa kimataifa wa Italia amefanikiwa kuiweka Napoli kwenye kilele cha msimamo wa ligi kuu nchini Italia kwa pengo kubwa la alama.
Kocha Spalletti anaingia kwenye vitabu vya historia vya klabu hiyo baada ya kuiwezesha Napoli kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa ulaya kwa mara ya kwanza, Hii inaendelea kuonesha namna gani kocha huyo amekua kwenye wakati mzuri kwenye klabu hiyo.
Napoli msimu huu wamekua moja ya timu tishio sio tu ligi ya Italia bali hata barani ulaya kwani wamekua wakishinda michezo yao kwa staili ya aina yake, Hii inaonesha namna kocha Luciano Spalletti amefanikiwa kuijenga timu hiyo na kuifanya kua timu shindani zaidi huku mpaka sasa ni moja ya timu zinazopewa nafasi sana ya kutwaa taji la ulaya.

