Alcaraz atwaa Rolland Garros mbele ya Sinner

Carlos Alcaraz amefanikiwa kumshinda bingwa namba moja Duniani Jannik Sinner kwenye mchezo wa fainali wa grand slam, uliochezwa hapo jana mjini Paris, Ufaransa.

Alcaraz atwaa Rolland Garros mbele ya Sinner

Alcaraz ambaye anashika namba mbili kwa ubora, aliibuka bingwa kwa ushindi wa jumla wa seti 4-6, 6-7, 6-4, 7-6, 7-6 baada ya pambano la Zaidi ya masaa matano na dakika 29, ikiwa ni fainali ya pili ndefu Zaidi kwenye historia ya fainali za grand slam.

Licha ya kuwa nyuma kwa seti mbili na kuzidiwa point tatu za ubingwa kutoka kwa Sinner, katika seti ya nne Alcaraz alionyesha ushujaa wa hali ya juu kwa kuokoa point hizo muhimu kabla ya kusawazisha na hatimaye kushinda pambano hilo kwa kishindo kupitia super-tie break ya seti ya mwisho.

Alcaraz atwaa Rolland Garros mbele ya Sinner

Ushindi huo ulimuwezesha Muhispania huyo kutetea ubingwa wake wa Roland Garros na kufikisha jumla ya mataji matano ya grand slam kwenye rekodi ya uchezaji wake.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa.

Sinner ambaye alikua na rekodi ya ushindi wa mfululizo mara 20 kwenye michuano mikubwa kabla ya mchezo huo, alionekana kukaribia kuliongeza taji la Roland Garros kwenye kabati lake la mataji baada ya lile la US Open na Australia Open. Licha ya kuongoza kwa seti mbili mapema na kuwa karibu na ushindi, alijikuta akipokea upinzani wa hali ya juu kutoka kwa Alcaraz na kushindwa kuulinda ushindin aliokua nao.

Alcaraz atwaa Rolland Garros mbele ya Sinner

Mchezo huo ulikua wa kwanza kwa Sinner kucheza kwa muda mrefu Zaidi hali iliyomfanya kuchoka sana na kufikia hatua ya kutumia kinywaji cha kulegeza misuli lakini bado jitihada zote hizo zilishindwa kumpa matokeo kwani Alcaraz alionekana kuwa mwenye utimamu wa hali ya juu na kufanya mashambulizi ya nguvu na kuvuruga mipango ya Sinner.

Baada ya kutamatika kwa mchezo huo, Alcaraz alikiri kwamba huo ndo mchezo wake mkubwa Zaidi kuwahi kucheza maishani mwake huku ukiwa na hisia za hali ya juu kutokana na kiwango kikubwa cha mpinzani wake huyo.

Alcaraz atwaa Rolland Garros mbele ya Sinner

“Leo ilikua mechi ya kipekee, ilikua na kila aina ya hisia, nyakati ngumu haswa lakini najivunia kwa namna nilivyokabiliana na changamoto zote za mchezo huu” alisema Alcaraz.

Alcaraz baada ya mchezo huu anakua miongoni mwa wacheza tennis waliopata mafanikio makubwa sana kwenye mchezo huo huku wakiwa na umri mdogo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.